Wakati
wakandarasi walipokuwa wanajenga daraja hili katika eneo la Miangalua
kwenye barabara ya Tunduma-Sumbawanga mwaka 2011. Barabara hiyo sasa
imekamilika.
Barabara
ya Mwanza-Musoma iko katika hali nzuri.
Ujenzi wa
barabara ukiendelea katika baadhi ya miradi nchini.
Ujenzi wa
barabara ya Iringa-Dodoma umekamilika kwa asilimia 95, bado maeneo machache
tu likiwemo hili la Mlima Nyang'oro ambapo Wachina wameuchonga ili
kupunguza kona katika umbali wa kilometa 15. (Picha zote na Daniel Mbega wa
www.brotherdanny.com
).
Na
Daniel Mbega, brotherdannyblog
Sumbawanga:
NAJIWEKA vyema kwenye
kiti na kutazama nje kupitia dirishani. Japokuwa giza limetanda majira haya
ya
saa 4:30 usiku, lakini ninaweza kuhisi jinsi basi hili nililopanda la
kampuni
ya Majinjah linavyotafuna lami.
Abiria
mwenzangu wa jirani ananiambai tutaingia
saa sita kasoro usiku mjini Sumbawanga mjini. Nafarijika japo uchovu ni
mwingi, maana kuketi kwenye basi kwa saa takriban 15 siyo mchezo ingawa
tulipata nafasi mara kadhaa za kupumzika 'kuchimba dawa' na kupata
mlo.
“Barabara yote
ni lami tupu ndugu yangu,
kasoro tu ni haya matuta kutoka Tunduma hadi Sumbawanga, lakini yamesaidia
kupunguza mwendokasi,” ananieleza.
Tunduma
tumeondoka kama saa tatu hivi
kuzikabili kilometa 222 hadi Sumbawanga, lakini safari hii ya kutoka Dar es
Salaam inayokadiriwa kuwa na umbali wa kilometa 1,000 imekuwa siyo ndefu
licha
ya uchovu wa kiuno na mgongo kutokana na kuketi tangu saa 12 alfajiri.
Faraja pekee
ni kwamba ninatumia siku moja tu kufika Sumbawanga, tofauti na miaka mitano
iliyopita ambapo nililazimika kutumia siku mbili huku nikiingia gharama za
ziada za kulala Lodge pale Mbeya kutokana na kutokuwepo na usafiri wa
uhakika kutokana
na ubovu wa barabara.
Wakati huo,
ukilala Mbeya unalazimika tena
kuamka mapema kuwahi basi ambalo licha ya kuondoka saa 12 alfajiri, bado
litafika Sumbawanga saa 8 mchana.
Jirani yangu
ananiambia kwamba sasa unaweza
kwenda na kurudi Sumbawanga mara mbili ukitokea Mbeya kwani mabasi ni mengi
na
njia ‘inateleza’.
“Wametukomboa
sana, magari hayajazi kama
zamani, unasafiri kwa raha na kwa wakati – muda wowote unaotaka,”
ananieleza.
Ndiyo.
Nakumbuka safari moja wakati
nikitokea Sumbawanga jinsi basi lilivyokuwa limejaza abiria mpaka sehemu ya
kupita ikakosekana. Walioketi walikuwa wachache kuliko waliosimama, sasa
piga
hesabu lilikuwa na abiria wangapi! Hata kondatka mwenyewe alilazimika kupita
kwa kuinama juu ya siti ili kwenda nyuma kuwapanga abiria waliosimama na
kuchukua nauli. Ilikuwa ni hatari.
Lakini leo
barabara hii imetandikwa lami na
imekuwa sehemu ya barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 6,276 ambazo
zimetengenezwa na utawala huu wa Awamu ya Nne, huku sehemu kubwa yabarabara
hizo ikiwa imesimamiwa na Dk. John Pombe Joseph Magufuli kama Waziri wa
Miundombinu.
Nimezunguka
karibu nchi nzima nikifanya habari za uchunguzi kwa miaka kumi iliyopita.
Mazingira ya wakati ule na ya sasa ni tofauti kabisa, maeneo ambayo
yalikuwa hayafikiki, hivi sasa hali ni nzuri.
Tangu Januari
hadi Juni 2015 pekee nimezunguka karibu kilometa 20,000 hapa nchini.
Nimezunguka nikitokea Iringa kwenda Arusha kupitia Dodoma-Singida hadi
Manyara; nimezunguka kutoka Dar es Salaam-Kiteto-Kondoa hadi Babati;
nimepita Babati-Kondoa-Mayamaya hadi Dodoma; nimepita
Mwanza-Shinyanga-Tabora-Mpanda hadi Sumbawanga mpaka Mbeya; nimetoka Dar es
Salaam-Njombe-Songea hadi Mbambabay; nimetoka Mwanza-Musoma hadi Sirari;
nimezunguka Mwanza-Sengerema-Geita hadi Bukoba; nimetoka Bukoba kupita
Kahama hadi Dar es Salaam; nimetoka Shinyanga-Maswa-Bariadi hadi Lamadi; na
maeneo mengine mengi kwa miezi sita.
Hakika
nilichokiona kinastahili kupongezwa kwamba kimefanyika. Ingawa barabara
kadhaa zimesimama kutokana
na kukosekana kwa fedha kufuatia msukosuko wa wafadhili kushindwa kutoa
fungu,
lakini nyingi kati ya hizo zimekamilika na kuiunganisha vyema
Tanzania.
Nilipita wakati
fulani ilipoanza
kutengenezwa barabara hii, nadhani ilikuwa mwaka 2011 nikiwa katika harakati
zangu za kuandika habari za maendeleo vijijini. Barabara hii ilimegwa katika
vipande vitatu ili kuharakisha ujenzi wake na kuzingatia
ubora.
Kipande cha
kwanza kilikuwa kutoka Tunduma hadi
Ikana chenye urefu wa kilometa 63.2 ambacho kilijengwa na kampuni ya
Consolidated
Contractors Group kwa gharama ya Dola 82.521
milioni; Kipande cha pili chenye urefu wa kilometa 64.2 kilikuwa kutoka
Ikana
hadi Laela na kilijengwa na kampuni ya China Newera (64.2km Ikana-Laela) kwa
Dola 46.812 milioni; na kipande cha mwisho kilikuwa kutoka Laela hadi
Sumbawanga chenye urefu wa kilometa 95.31 ambacho kilijengwa na kampuni ya
Aarsleff-Interbeton J.V kwa gharama ya Dola 130.038 milioni. Kwa hiyo
kilometa zote 222.71 ziligharimu jumla ya Dola 259.371 milioni ambazo ni
fedha
za wahisani na fedha za ndani.
Ni
fedha nyingi sana lakini haziwezikuzidi thamani halisiya barabara hii ambayo
licha ya kuwakomboa wananchi wa pembezoni hasa katika mikoa ya Mbeya, Rukwa
na
Katavi, lakini pia itasaidia kuiunganisha Tanzania na nchi jirani ya
Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo kwa sababu ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa
112
kutoka Sumbawanga-Matai hadi bandari ya Kasanga katika Ziwa Tanganyika
unaendelea chini ya kampuni ya China Railway 15th Bureau
Group Corporation - CR15G kwa gharama ya Dola 80.912
milioni.
Dk. Magufuli, ambaye sasa
ni mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), anazifahamu karibu
barabara
zote nchini na hatua zilikofikia. Alipoingia kwa mara ya kwanza bungeni
mwaka