MIAKA 53 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA VAZI LA TAIFA NI LIPI

Miaka 53 ya muungano Kauli mbiu ni  tuulinde na kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na kuwajibika na kufanya kazi kwa bidii.

Stara Thomas, mwimbaji wa zouk akiwa amevalia vazi murua kabisa!
Picha: hisani ya haki-hakingowi blog.

Katika kuadhimisha miaka 53 ya uhuru ni vema pia tukikumbuka kutafuta vazi ambalo linatutambulisha kama watanzania kama mataifa mengine yanavyojitambulisha kupitia maleba hata wanayovaa katika kazi zao za sanaa.Nimejaribu kuonesha baadhi ya picha ambazo watu wanajaribu kuonesha asili yao kwa kuvaa nguo zenye rangi ya bendera ya Taifa ili kuonesha uzalendo.

Msanii wa mashairi ya kughani akionesha uzalendo kwa kuvaa cheni ya kichwani yenye rangi za bendera ya Taifa.


Msanii Diamond akiwa na wasanii wengine ambao waliungana kutengeneza wimbo wa muungano,Lakini nia yangu  katika picha hii nikuonesha ambavyo wasanii hawa wanashauku ya kuwa na vazi la taifa na wanapokosa basi wanatumia vitambaa kuonesha uzalendo lakini bado haitoshi,nadhani serikali inatakiwa kuangalia pia suala la vazi la taifa kwani mpaka sasa ni suala Mtambuka.


 

 
Maoni yangu ni kwamba suala la kila mwananchi kujiamulia vazi la kuvaa sisahihi hata kama tunatofautiana kimazingira,basi vazi hilo liangaliewe katika hali ya rangi au kitambaa ambacho kila mwananchi anaweza shina nguo na kuvaa pahala popote.

 Historia ya Muungano

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa mnamo tarehe 26 Aprili, 1964 kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja). Tanganyika ilikuwa ni mwendelezo wakoloni la Ujerumani, utawala wa Waingereza kwa Mamlaka ya Umoja wa Mataifa, Himaya ya Umoja wa Mataifa chini ya utawala wa Uingereza na mwisho Taifa huru kuanzia mwaka 1961 ndani ya nchi za Jumuiya ya Madola.
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkataba huu wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume tarehe 22 Aprili 1964 huko Zanzibar. Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi hapo tarehe 26 Aprili, 1964 na mnamo tarehe 27 Aprili, 1964, viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar esSalaam na kubadilishana Hati za Muungano. Sheria za Muungano zilitoa tamko la Jamhuri ya Muungano katika Ibara ya 4 kwamba:

“Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitalazimika, baada ya kuungana na siku zote baada ya kuungana, kuunganishwa kuwa Dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar’ (Ibara ya 4 Sheria za Muungano)”
Jina hili la “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar” lilibadilishwa baadae mnamo tarehe 28 Oktoba, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post