Mkurugenzi
Idara ya Uratibu wa Shughuli za serkali Obey Assery akisistiza jambo
wakati wa Mkutano wa wadau wa MIVARF Agosti 30, Agosti, 2017 mjini
Dodoma.
Wataalamu
kutoka Program ya MIVARF wakifuatilia majadiliano ya wadau wa Program
hiyo wakati wa mkutano wa wadau wa MIVARF Agosti 30 Mjini Dodoma.
Baadhi ya wadau wa MIVARF wakifuatilia mkutano wa wadau wa MIVARF unaofanyika mjini Dodoma Agost, 2017.
Programu
ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji thamani na Huduma za Kifedha
Vijijini(MIVARF), imefanikiwa kupunguza umasikini wa kipato na
kuimarisha uhakika wa chakula katika Halmashauri 73 zinazotekeleza
program hiyo kwa Tanzania Bara na Visiwani.
Akiongea
wakati wa Mkutano wa wadau wa MIVARF wa siku mbili tarehe 29 hadi 30,
Agosti, 2017 mjini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya uratibu wa shughuli
za serikali Ofisi ya Wazir Mkuu, Obey Assery alifafanua kuwa lengo la
Program hiyo inalenga kuongeza uzalishaji na tija kwa walengwa.
“Program
imelenga kuwajengea uwezo wazalishaji ambao huwa katika vikundi kwa
kuvifiki vikundi 2,331 vyenye walengwa 81,677. Kimsingi Programu
imelenga kumuwezesha mkulima aweze kufanya kilimo cha kibiashara”
alisema Assery.
Naye
Mratibu wa Program Kitaifa, Walter Swai alibainisha kuwa Program
imelenga kuwajengea uwezo walengwa kuyafikia masoko ya uhakika ili
waweze kupunguza umasikini wa kipato.
“Programu
imelenga kuboresha 1,000km za barabara hadi sasa 9991.8km
zimeshakamilika sawa na asilimia 92. Lakini pia kwa upande wa miundo
mbinu ya masoko tunajenga maghala, hadi sasa kati ya maghala 29 yaliyo
kwenye malengo tayari tumekamilisha maghala 24 sawa na asilimia 83 ”
alisistiza Swai.
Swai
aliongeza kuwa Program hiyo imepanga kukarabati maghala 6 ambapo tayari
yote yamekamilika, pia tumelenga kujenga masoko 16 ambapo hadi sasa
masoko 7 yamekamilika ambayo ni asilimia 44.
MIVARF;
ni Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini
iliyobuniwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa
Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo yaani (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya
Afrika (ADB).