Na Woinde Shizza , ARUSHA
Ikiwa katika baadhi ya Mila na tamaduni za kiafrika zinaonyesha kuwa mwanamme anawajibu wa kuhudumia familia akiwa kama baba na kichwa cha familia lakini katika baadhi ya wanaume wa kabila la kimasai na waarusha kwao imekuwa tofauti kwani wengi wao wamekuwa wakiwaacha wanawake kuchukua jukumu la kulea watoto na kuhudumia familia.
NINI TATIZO
Tatizo hilo la wanawake kuachiwa majukumu ya kulea watoto na familia kwa ujumla limewakumba baadhi ya wanawake wa kimasai na mwandishi wa habari hizi alizungumza na baadhi ya waishio katika wilaya ya Arumeru ndani ya halmashauri ya Arusha ambao mwandishi wa habari hizi alibahatika kuonana nao na kueleza kilio chao huku baadhi yao wakikiri kuwa wao wanachukulia kama sehemu ya tamaduni kwani tangu enzi za mabibi zao walikuo wanashuhudia wanawake wakiangaika kutunza familia
Pia kwa uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa makala hii ulibaini kuwa Wamasai wana
upendo wa kimila uliopitiliza ambao hauwezi kuonekana kwa makabila mengine kwa
sababu hufanyika katika mazingira ya siri ili kuzuia usumbufu na kero.
Nakwetu Sindio ni mama wa watoto watatu ambaye anaishi katika kijiji cha oldonyosambu wilayani Arumeru mkoani Arusha anasema kuwa mwanamume wake amekuwa ajali familia kabisa kwani anamuachia yeye majukumu yote ya kulea familia
"Unajua hawa wanaume wetu wamekuwa wamejijengea hii tabia toka mda mrefu nadhani tangu enzi za mama zetu na sisi tumeona kama ni Mila kwani tangu babu zetu wanaume wakimasai walikuwa wanaakikisha tu mwanamke anaemuoa anakuwa na sehemu ya kuishi yaani nyumba ,na mbaya zaidi yeye akishampa mwanamke sehemu ata iwenyumba ya nyasi anakuwa amemaliza atamzalisha mwanamke lakini akishamzalisha ataki kujua chochote zaidi ya kuja alale na chakula anataka akute lakini atoi matumizi yeyote"
"Mfano Mimi nimezalishwa mwanamme wangu ameenda uko Nairobi anasema ameenda kutafuta maisha lakini chakushangaza amna ata ela ambayo anatuma Kwa ajili ya watoto Mimi ndio nitembeze ivi viazi vyangu niuze nipate ela watoto wale na sasa ivi nina miaka 28 Nina watoto wanne yaani yeye kisa amanioa na kuniweka katika boma yake anakazi ya kunizalisha na kuondoka jukumu la kulea watoto ameniachia Mimi"alisema Neema Saigueani
NINI KINAWASAIDIA HADI WANAMUDU KULEA FAMILIA
Sara Emanuel anaeleza kuwa kitu kikubwa ambacho kinawasaidia hadi wanaweza kulea familia ni kwamba asilimia kubwa ya wanawake wa jamii ya kifugaji wanapenda kujishughulisha hawachagui biashara ya kufanya wao wanalima, wanafuga ,wanatembeza vitu mbalimbali kama viazi ,mboga ,mahindi na vingine Kwa ajili kuwauzia watu mbalimbali
"Unajua ukichunguza wanawake wengi wa jamii ya kifugaji utagundua kuwa ni wanawake wanaopenda kujishughulisha ata ukiangalia uko masokoni wanaouza vitu wale wanaotembeza vitu nao pia ni wamasai na wengi wao ukichunguza historia yao utagundua kuwa wanatafuta Kwa ajili ya kulea watoto wao maana wanaume zao hawawasaidiu kwani
wanaamini kuwa ukishampa nyumba mahali pa kukaa jukumu la kulea watoto ni mama.
NINI KIFANYIKE ILI WANAUME HAWA WABADILIKE WATAMBUE JUKUMU LAO
-Wanawake hawa wameziomba taasisi zisizo za kiserikali (NG'O) kusaidia kuwapa elimu wanaume wao ya juu ya kutunza na kulea familia zao ili kuweza kuwasaidia kupunguza majukumuni ya kulea familia wanawake zao
-kwa wale baadhi ya wanaume wa jamii ya kifugaji ambao angalau wamepata elimu na wanajitambua watumie majukwaa yao ya kimila kuwahamasisha wale wengine ambao hawasaidii majukumu ya kulea watoto kutambua faida za kumsaidia mwanamke kulea watoto kwani wanavyowaachia wanawake wenyewe muda mungine yanawazidi na kusababishia wengine kujiingiza ata katika tabia mbaya za umalaya ambazo zitawapelekea kupata magonjwa
-Serikali itenge fedha Kwa ajili ya kupiga kampeni za kutoa elimu kwa jamii hiiyo ya juu ya umuhimu wa baba kutunza familia na kushirikiana na mama kulea familia na sio kukumuachia mama huku maafisa ustawi wa jamii waandae madarasa Kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanaume na kuwaondolea Ile dhana potofu ya kusema jukumu la kulea watoto ni lamwanamke mwenyewe.