RAIS WA CHAMA CHA MAHAKIMU NA MAJAJI: “ASASI ZA KIRAIA NI NGUZO YA HAKI NA UWAJIBIKAJI”

 



Wakichangia mjadala huo, baadhi ya wakurugenzi wa asasi ya kiraia walisema kuongezeka kwa matukio ya ukatili kunachangiwa pia na kuachiwa huru kwa watuhumiwa, kupewa dhamana watuhumiwa.



Mratibu wa kitaifa wa Mtandao wa watetezi wa haki za binaadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo ole Ngurumwa alisema ni kweli kuna haja ya kifanyika utafiti juu ya makosa ya kujamiiana na adhabu zake



Wakili Ole Ngurumwa alisema miongoni mwa mambo yanahitaji mjadala ya utafiti ni suala la dhamana kwa watuhumiwa.



"Ingawa sisi kama watetezi tunatakiwa kufanya utetezi makosa yote yawe na dhamana na kama dhamana isipotolewa itokane na maamuzi ya hakimu ama Jaji na sio sheria kukataa"alisema



Mkurugenzi wa Shirika la Paralegal Primary Justice (PPJ) Gabriel John alishauri kesi za makosa ya kujamiiana zisichukuwe muda mrefu ili wakosaji walipate muda kukwepa adhabu.


Mkurugenzi la Youth Against HIV/AID and Poverty Alex Luoga alisema kuongezeka kwa makosa ya kujamiiana kunachangiwa na baadhi ya maamuzi yasiyo rafiki ya Mahakama na umasikini kwani wanaotendewa wanashindwa kufikisha mashauri mahakamani na kufatilia kesi.


Mkurugenzi wa Shirika la Nguruka Development Agency (NDA) Samweli Nsokolo alishauri kuimarishwa ushirikiano baina ya Azasi za Kiraia, Mahakama, Vyama vya Mawakili 


Katibu wa Chama cha Mawakili wa Afrika ya Mashariki (EALS) Wakili John Seka kuna haja ya Asasi za Kiraia kujengewa uwezo masuala ya kisheria ili ziweze kusaidia jamii.


Hizi hapa takwimu za ongezeko makosa ya kujamiiana.    


Uchungunzi uliofanywa na MAIPAC kutoka taarifa rasmi serikalini na kwenye asasi za kiraia zinaonesha   makosa ya kujamiiana nchini yana  mwelekeo wa kuongezeka  katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. 

Hapa chini ni muhtasari wa takwimu zilizopatikana kwa kipindi cha 2015 hadi 2023:


-l

Takwimu  zinaonesha kati ya mwaka 2015–2018

- *Ubakaji* 

  - 2015: Matukio 5,802

  - 2016: Matukio 7,645

  - 2017: Matukio 8,039

  - 2018: Matukio 7,617


- *Ulawiti* 

  - 2015: Matukio 928

  - 2016: Matukio 1,202

  - 2017: Matukio 1,184

  - 2018: Matukio 1,201

*2019–2022*

- *Ubakaji:*

  - 2019–Machi 2022: Jumla ya matukio 19,726 kati ya matukio 27,838 ya ukatili wa kijinsia yaliyoripotiwa.

*2022–2023*

- *Ubakaji:*

  - 2022: Matukio 6,827

  - 2023: Matukio 8,691

- *Ulawiti:*

  - 2022: Matukio 1,586

  - 2023: Matukio 2,488

- *Watoto Walioathirika na Ulawiti:*

  - 2022: Watoto 1,555

  - 2023: Watoto 2,382 (ongezeko la 53%)


 Mikoa Inayoongoza kwa Matukio


- *Ubakaji:* Mjini Magharibi (Zanzibar) na Morogoro

- *Ulawiti:* Arusha na Mjini Magharibi



Mafunzo hayo yameandaliwa na Mtandao wa  Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS), Umoja wa Wanasheria wa Afrika (PALU), na Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) kwa udhamini wa  Umoja wa Ulaya.


About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia