Nondo Oscar Awasha MOTO wa Ubunifu kwa Vijana"

 

Mfugaji na mfanyabiashara wa mbwa, Nondo akionyesha moja ya mbwa anaowauza

Na Woinde Shizza, Arusha 

Mfugaji na mfanyabiashara wa mbwa, Nondo Oscar, mkazi wa jiji la Arusha, ameibuka kuwa mfano wa kuigwa baada ya kufanikisha biashara inayomuingizia hadi Sh milioni 30 kwa kuuza mbwa mmoja.


Oscar, anayefuga mbwa wa aina mbalimbali, amesema biashara hiyo ndiyo chanzo kikuu cha kipato chake na imebadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa. Alieleza kuwa awali alikuwa akijihusisha na biashara nyingine ambazo hazikumlipa vizuri, lakini kupitia ufugaji wa mbwa ameona matunda ya kujituma.

“Nimekuwa nikifanya biashara hii kwa miaka kadhaa sasa na imenisaidia sana kiuchumi. Kijana ukijituma hakuna kazi mbaya, ajira zipo kwa wale wasiokuwa wavivu. Wanaolalamika kwamba hakuna ajira mara nyingi ni wavivu,” alisema.


Mbali na kufuga, Oscar pia hufundisha mbwa wake kwa mafunzo mbalimbali na kuwakaribisha wananchi kutembelea banda lake ili kujionea. “Tunakaribisha wateja kununua mbwa wa aina zote hapa Arusha. Tunatoa pia huduma ya kufundisha mbwa,” aliongeza.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya kilimo ya Nane Nane yanayoendelea jijini Arusha, Oscar aliwataka vijana kuwa wabunifu na kutokuchagua kazi, akisisitiza kuwa kila mtu anaweza kufanikisha maisha yake iwapo ataacha kulalamika na kuanza kufanya kazi kwa bidii.

076350000 kwa mahitaji ya mbwa

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia