Kampuni ya Ulinzi ya Kashai KS Security Yatoa Wito kwa Wananchi Kuhakikisha Usalama wa Mali Zao
Na Woinde Shizza, Arusha
Katika mwendelezo wa Maonesho ya 31 ya Kilimo na Mifugo yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro jijini Arusha, kampuni ya ulinzi ya Kashai KS Security imewataka wananchi kuchukua hatua za makusudi za kulinda usalama wa nyumba, ofisi na kampuni zao kwa kutumia huduma za ulinzi zilizo rasmi na zenye kuaminika.
Akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao, Mkurugenzi wa Masoko wa Kashai KS Security Twaha Rashid , amesema kuwa kampuni hiyo imekuja katika maonyesho hayo si kwa ajili ya kutangaza huduma pekee, bali pia kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuwa na mipango madhubuti ya kiusalama hasa nyakati hizi ambazo vitendo vya uhalifu vimekuwa vikishika kasi katika baadhi ya maeneo ya nchi.
“Tunahamasisha wananchi, wafanyabiashara na taasisi mbalimbali kuhakikisha wanatumia huduma halali za ulinzi kama njia ya kudhibiti matukio ya wizi na uvamizi , Kashai KS Security tupo tayari kuwahudumia kwa weledi na kwa gharama nafuu,” amesema
Amesisitiza kuwa usalama ni jambo la msingi kwa maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla, na kwamba kutokuwa na utaratibu mzuri wa ulinzi ni kuruhusu hatari kwa familia, wafanyakazi na mali zilizopo.
Ametumia nafasi hiyo kuwaalika wananchi kutembelea banda lao lililopo kwenye viwanja vya Nane Nane Themi Njiro kwa ajili ya kupata maelezo zaidi kuhusu huduma wanazotoa, ikiwemo ulinzi wa makazi ya watu binafsi, taasisi, maeneo ya biashara, pamoja na ulinzi wa shughuli mbalimbali za kijamii.
“Tuna walinzi waliopitia mafunzo ya kitaalamu, tuna vifaa vya kisasa na tuna mfumo mzuri wa ufuatiliaji usiku na mchana, Usisubiri hadi tukio litokee ndipo uchukue hatua bali Linda unachokimiliki mapema,” amesisitiza.
Aliwataka Wananchi kuzingatia usalama wa maisha na mali zao kwa kushirikiana na kampuni za ulinzi zilizosajiliwa na kuthibitishwa na vyombo husika, huku wakihimizwa kuchukua hatua mapema kabla y
a madhara kutokea.



0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia