Ticker

6/recent/ticker-posts

KATIKA KUDHIBITI BIASHARA HARAMU YAWANYAMAPORI NCHI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA

 Na Queen Lema, Arusha

Naibu Waziri mali asili na utalii ataka umoja na ushirikiano baina ya nchi, na nchi katika kudhibiti biashara haramu ya wanyamapori. 



Taasisi mbalimbali ambazo zinasimamia na kudhibiti biashara haramu za wanyama pori zimetakiwa kuongeza umoja pamoja ushirikiano ili kudhibiti wimbi la biashara haramu ya wanyamapori ambayo inaendelea kwenye baadhi ya nchi. 



Aidha biashara hiyo pia imekuwa ikisababisha madhara mbalimbali kama vile ukosefu wa kodi, ushuru, na hata usalama wa wanyama kwa kuwa hata njia ambazo zinatumika huwa ni njia za kujificha 



Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa Mali asili na utalii, Dunstan Luka wakati akifungua mafunzo ya kikanda juu ya kukabiliana na usafirishaji haramu wa wanyamapori kati ya Afrika na Asia. 


Waziri huyo alisema kuwa nchi za Afika na Asia zimefanikiwa kubaraikiwa kuwa na maliasili pamoja na wanyama ambao ni vivutio 


Alisema kuwa pamoja na kuwa nchi zinebarikiwa lakini bado kuna genge kubwa la baadhi ya wananchi au raia kutoka nchi jirani kufanya biashara haramu za wanyama hasa kwa kupitia mipaka baina ya nchi na nchi 



"haya mafunzo ni muimu sana kwa maendeleo ya nchi na nchi lakini pia kuhakikisha kuwa jitiada na makubiliano ambayo yalifanyika kule lusaka yafuatwe, ila ili yaweze kufanikiwa kunaitajika ushirikiano mipakani ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo baina ya nchi na nchi"aliongeza"alisema


Akiongelea hali ya biashara haramu kwa Tanzania alisema kuwa hali hiyo imepungua kwa kiwango kikubwa sana tofauti na hapo awali ambapo biashara haramu ya wanyama pori ilishamiri. 


"Tanzania imepiga hatua kubwa sana hasa kwenye biashara haramu lakini hata usafirishaji haramu wa wanyama ambao ni rasilimali za taifa bado tunaendelea kupigania maslahi ya taifa kwa kuwa biashara haramu inachangia kwa kiwango kikubwa kushusha hata maslai ya taifa"aliongeza


Akiongea kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo Wakili Salimu Msemo alisema kuwa mafunzo hayo ambayo yameshirikisha nchi mbalimbali yataweza kuwasaidia endapo kama kutakuwepo na umoja baina ya nchi na nchi,mipaka na mipaka, sanjari na kuwepo kwa mbinu za upelelezi ambazo zitaweza kuwanasa wahalifu kwa haraka



Post a Comment

0 Comments