CPA. MAKALLA AINGIA ARUSHA KWA KISHINDO
Mkuu wa mkoa wa Arusha CPA.Amos Makalla akipokelewa Leo alipowasili ofisini kwake
Kauli hiyo imetolewa na mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, CPA. Amos Gabriel Makalla, wakati wa hafla ya mapokezi yake iliyofanyika leo kuanzia saa mbili asubuhi katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ambapo mamia ya wananchi walijitokeza.
Makalla alisema ataendeleza mazuri yote yaliyofanywa na watangulizi wake na kuongeza msisitizo katika maeneo muhimu ya maendeleo yakiwemo utalii na michezo.
“Arusha ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo heshima ya mkoa huu lazima iendane na hadhi hiyo, Tutaendeleza utalii, lakini pia tutaweka mkazo kwenye utalii wa michezo.
" Haiwezekani kuwa na uwanja mkubwa bila kuwa na timu ya ligi kuu ,uwanja wa Mpira ambao mashindano ya AFCON yatachezwa hapo unajegwa Hapa lakini nashangaa Amna timu ya Mpira mkoani apa , Nataka Arusha iwe kinara katika michezo na utalii wa michezo nchini,” alisema Makalla.
Aidha, alisisitiza kuwa mafanikio ya maendeleo hayawezi kupatikana bila kuwepo amani na mshikamano wa wananchi.
“Ninachukia uzembe Mimi ni mtu wa kazi Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, na viongozi wote wa taasisi lazima wafanye kazi kwa ufanisi Wananchi ndio mabosi wetu, tunapaswa kusikiliza na kutatua kero zao Nitawafuata viongozi popote walipo ili kuhakikisha kazi inafanyika pamoja na kutatua kero za wananchi,” aliongeza.
Makalla alisisitiza ushirikiano wa pamoja baina ya wananchi na viongozi, akisema hakuna jambo linaloshindikana iwapo ushirikiano utadumishwa.
Mmoja wa viongozi wa dhehebu la Bohora Hassan Mulla akiongea na waandishi wa habari juu ya ujio wa mkuu wa mkoa wa Arusha Kwa upande wake, Hassan Mulla, mmoja wa viongozi wa dhehebu la Bohora jijini Arusha, alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani na mshikamano wa kitaifa.
“Wananchi tunapaswa kulinda amani yetu amani ndiyo msingi wa maendeleo na bila utulivu hakuna kinachoweza kufanikishwa,” alisema.
Mulla aliongeza kuwa uchaguzi mkuu ni tukio la kidemokrasia linalopaswa kuleta mshikamano na siyo mifarakano.
“Ni jukumu letu sote kuhakikisha kuwa kampeni na uchaguzi vinapita kwa amani ,tukilinda amani, tutajipatia maendeleo na vizazi vyetu vitajivunia, Viongozi wa dini na taasisi zote lazima tuungane kusisitiza hili kwa wananchi,” alieleza.
Alisema jamii ya Bohora kwa muda mrefu imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na serikali na wananchi wengine kulinda utulivu wa taifa, na itaendelea kushirikiana na uongozi mpya wa mkoa kuhakikisha Arusha inabaki kuwa kitovu cha amani na maendeleo.






0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia