ZUBERY MWINYI WA CUF ATANGAZA AJENDA YA KUINUA VIJANA WASIO NA AJIRA
Na Woinde Shizza , Arusha
Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Zubery Mwinyi, amechukua rasmi fomu za kugombea nafasi hiyo leo, mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Shaban Manyama.
![]() |
| Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Shaban Manyama akimpa maelekezo mgombea |
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu, Zubery amesema dhamira yake kuu ni kuwasaidia wananchi wa Arusha Mjini, hususan vijana wasio na ajira, kwa kuweka mipango ya kuongeza fursa za kiuchumi na ajira endelevu.
“Vijana wengi wa Arusha wana ari na uwezo, lakini wanakosa nafasi, Nikipewa ridhaa nitahakikisha tunafungua milango ya ajira na miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wote,” amesema Mwinyi.
Hatua hiyo inafanyika ikiwa ni siku ya pili tangu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ifungue rasmi dirisha la uchukuaji wa fomu za kugombea ubunge kwa vyama vya siasa nchini.
#KuraYakoHakiYako #JitokezeKupigaKura


0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia