EWURA YAWAHAMASISHA WANANCHI JUU MATUMIZI YA NISHATI SAFI


Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) mhandisi Lorivii Long'idu akiongea na waandishi wa habari Katika  maonyesho 31 ya wakulima(nanenane) ya kanda ya kaskazini  yanayofanyika ndani ya viwanja vya Themi njiro  

Na Woinde Shizza,Arusha

Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) mhandisi Lorivii Long'idu ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya matumizi ya nishati safi kupitia banda la EWURA katika Maonyesho ya 31 ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro, jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja huyo alisema EWURA inatumia fursa ya maonyesho hayo kuelimisha umma kuhusu majukumu yake, ikiwemo suala la upangaji wa bei za mafuta maeneo yote nchini, pamoja na kusimamia huduma za nishati na maji kwa mujibu wa sheria.


Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) mhandisi Lorivii Long'idu wa kushoto akiongea na mteja alieudhuria Katika banda lao lililopo Katika viwanja hivyo

Alisema kuwa moja ya malengo makuu ya EWURA ni kuhamasisha matumizi ya nishati safi, na kwamba mamlaka hiyo inashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mpango wa miaka 10 wa Serikali wa kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034, angalau asilimia 30 ya Watanzania watakuwa wamehama kutoka kwenye nishati isiyo salama na kutumia nishati safi kama gesi.

“ tunatumia fursa hii kusisitiza matumizi ya nishati safi siyo tu kwa ajili ya kulinda afya ya jamii, bali pia kwa kulinda mazingira, Tafiti zilizofanywa na shirika la afya duniani zinaonyesha kuwa magonjwa mengi ya mfumo wa upumuaji yanatokana na matumizi ya kuni na mkaa majumbani,” alisema.

Aidha, Meneja huyo alieleza kuwa EWURA inaendelea kusimamia kwa karibu usambazaji wa gesi kwa kuhakikisha wananchi wanauziwa gesi yenye ujazo sahihi kama ilivyopimwa.

 Alisema baadhi ya mawakala wa gesi wamekwisha kamatwa kwa kukiuka sheria, na baadhi ya kesi zao zipo mahakamani wanasubiria maamuzi yatolewe na yakisha tolewa watatoa taarifa ili iwe fundisho kwa wengine


“Ni jukumu la kila msambazaji mkubwa kuhakikisha wauzaji wadogo wanafuata sheria zote, na wananchi wanapaswa kuhakiki kuwa gesi wanayonunua imejaa kikamilifu na imepimwa vizuri,” alisisitiza.


Aidha aliwataka wananchi kufika katika banda la EWURA ili wapate elimu ya kina kuhusu huduma za nishati na maji, sambamba na kuwasilisha changamoto zinazohusu umeme, maji, mafuta na gesi, ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia