ASKOFU MANASSEH: TUMLILIE MUNGU, TULINDE AMANI

 Askofu Mkuu wa Kanisa la Baptist Tanzania, Dk. Arnold Manasseh, amewataka Watanzania wote kushirikiana kulinda amani ya taifa kwa mshikamano na maombi, bila kujali tofauti za dini, kabila au itikadi za kisiasa.



Akizungumza katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa darasa la saba, Askofu Manasseh alisema kila raia ana wajibu wa kuchangia mustakabali wa nchi, Aliongeza kuwa jukumu la kulinda amani haliwezi kuachiwa wanasiasa pekee bali kila mwananchi.

"Kwanza kabisa tunapaswa kumlilia Mungu bila kuangalia tofauti zetu Tunatakiwa kulinda amani ya nchi yetu, kwani tukiharibu wote tutanywea kikombe hicho bila kujali chama au dini," alisema huku akiwataka Watanzania kuungana kwa mshikamano.

Askofu huyo alionya kuwa changamoto za kisiasa na kijamii zinazojitokeza zinahitaji suluhisho la kiroho na mshikamano wa kitaifa ,Alisema maombi ndiyo yanayoweza kubadilisha hali ya taifa, kurejesha mshikamano na kuleta utulivu wa kudumu.


Aidha, Askofu Manasseh aliwataka wazazi na walezi kutumia kipindi hiki kujenga maadili ya watoto ,Alisisitiza kuwa tatizo la mmonyoko wa maadili limekithiri katika jamii na linahitaji juhudi za makusudi kukabiliana nalo.

"Wazazi wa sasa wanapaswa kuwa walimu wa kwanza wa maisha Kwanza wawekeze kwa Mungu, kisha katika elimu, Tukiwafundisha kufanya kazi kwa bidii na kumuweka Mungu mbele, tutakuwa tumewaandaa kwa maisha bora," alisisitiza.

Kwa upande wake, Meneja wa shule hiyo, Lambert Hassan, alisema jumla ya wanafunzi 60 wa darasa la saba wamehitimu mwaka huu na kupongeza mshikamano wa walimu, wazazi na jamii. 

Alisema mahafali hayo yanaonyesha dira ya shule katika kuandaa watoto kuwa raia wema na wachapa kazi.

"Mahafali haya ni matokeo ya mshikamano wa pamoja. Tunapaswa kuendelea kushirikiana ili kila mtoto apate mwongozo sahihi na motisha ya kufanya vizuri zaidi," alisema Hassan na kuwataka wazazi kuhakikisha wanawafuatilia watoto wao hata wanapokuwa likizo.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia