DK.SAMIA AACHA FURAHA PANGANI AKIOMBA KURA KUELEKEA OKTOBA 29
Aweka wazi mikakati wa kuifungua Pangani kwa miundombinu ya barabara
MGOMBEA
Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Rais Dk.Samia Suluhu
Hassan ametoa ahadi mbalimbali ambazo Serikali inakwenda kuyatekeleza
katika miaka mitano ijayo katika Wilaya ya Pangani mkoani Tanga huku
akitumia nafasi hiyo kuzungumza Ujenzi wa barabara ya
Bagamoyo-Saadan-Pangani hadi Tanga ambayo unaokwenda adha ya usafiri.
Akizungumza
na wananchi wa Wilaya ya Pangani katika mkutano wa kampeni kuelekea
Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu Dk. Samia amesema Februari mwaka huu
alifika Pangani kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Mto Pangani
na barabara ya Bagamoyo - Saadani - Pangani - Tanga.
Amesema kwa
muda mrefu wananchi wamekuwa wakisubiri barabara hiyo ambayo
itawaondolea adha ya kulazimika kusafiri masafa marefu kwa kukosa
muunganiko kati ya wilaya za Bagamoyo na Pangani.
"Barabara hii inaendelea vizuri na itakwenda kufungua ukanda wa Pwani kiuchumi na kupunguza gharama za usafiri na usafirishaji.
"Kwa
wale ambao hawajapata fursa ya kusoma Ilani naomba nigusie kwamba
tunapoanza na barabara hii kwa kipande cha Tanga - Pangani kilometa 50
ujenzi umefikia asilimia 75," amesema
Ameongeza kipande cha
Pangani - Saadani - Makurunge chenye kilometa 95 ujenzi umefikia
asilimia 50 huku daraja la Mto Pangani lenye mita 525 na barabara
unganishi imefikia asilimia 60.
Akieleza mbele ya wananchi hao
Dk. Samia amesema ahadi ya CCM kwa wananchi wa Pangani ni kuikamilisha
barabara hiyo ambapo siyo muda mrefu wananchi wataanza kufaidi matunda.
Kuhusu
uvuvi Dk.Samia amesema Serikali imewezesha upatikanaji boti 15
zinazosafiri kwa umbari mrefu baharini kwa shughuli za uvuvi wa dagaa na
samaki.
"Ninakumbuka nilizindua mradi huu wenye thamani ya Sh.
bilioni 1.6 ambao utaongeza fursa za ajira kwa vijana wetu. Sambamba na
hilo tumeanza ujenzi wa soko la samaki la kimataifa Kata ya Kipumbwi.”
Amefafanua
mradi huo wa sh. bilioni 1.3 utakuwa na vifaa vya kukaushia dagaa ni
muhimu katika kuwaongezea kipato wavuvi na kuchochea maendeleo ya wilaya
yetu.
Ameongeza katika awamu ijayo serikali kali yake itaendelea kuwashika mkono wavuvi ili kuongeza vipato vyao.
Akizungumza kuhusu wafugaji, amesema kwamba serikali itaendelea kuleta mageuzi sekta ya ufugaji kuwa ya kisasa.
“Kwa
Pangani serikali imetoa ng'ombe wa maziwa 51 huku kitaifa ikitoa ruzuku
ya chanjo bure kwa kuku na nusu bei kwa mifugo mingine."Hii tumeifanya
kupandisha thamani ya mifugo yetu. Tumehangaika kwa muda mrefu kutafuta
masoko ya kimataifa. Tumepata masoko makubwa.”


0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia