BULK YATOA HUDUMA BORA, WANANCHI WAFURAHIA PUNGUZO LA ASILIMIA 20% NA ZAWADI YA JIKO POA

 

Afisa Rasilimali Watu wa Bulk, Elias Joseph wapili kushoto akiongea na moja ya mteja alipotembelea dukani apo

Na Woinde Shizza, Arusha

Kampuni ya Bulk, inayojihusisha na uuzaji wa vifaa bora vya ujenzi hapa nchini, imeunga mkono maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kutoa punguzo la asilimia 20% kwa bidhaa zake mbalimbali, pamoja na kutoa zawadi ya jiko poa kila siku, hasa katika kipindi hiki cha wiki ya huduma kwa wateja.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo, Afisa Rasilimali Watu wa Bulk, Elias Joseph, aliwatahadharisha wananchi kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na ofa ya kipekee.

 Joseph alibainisha kuwa punguzo hili linahusisha bidhaa kama tailisi, masinki ya chooni na vifaa vingine vya ujenzi vinavyouzwa na kampuni hiyo, huku akisisitiza kauli mbiu ya kampuni hiyo “Less Shillings, More Value”.



“Tunawahimiza wananchi wote wajitokeze kupata bidhaa zetu bora, zenye viwango vya juu, hasa katika kipindi hiki cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Pia zawadi ya jiko poa ni njia yetu ya kuunga mkono kampeni ya Rais Samia ya kutumia nishati mbadala,” alisema Joseph.

Kampuni ya Bulk imejipanga kutoa bidhaa bora, zenye ubora wa hali ya juu, zinazokidhi viwango vya kimataifa, huku ikihakikisha wateja wanapata huduma za kiwango cha juu, zenye uwazi na uwajibikaji

Alisema huduma za Bulk si tu zinahakikisha bidhaa zinapatikana kwa wakati, bali pia zinatoa mwongozo kwa wateja kuhusu bidhaa bora za ujenzi na matumizi sahihi ya vifaa vyao, hii inajenga uhusiano imara kati ya kampuni na wateja wake, na kudumisha kielelezo cha kampuni inayowajali wateja wake kwa dhati.

Aidha, mmoja wa wananchi waliotembelea duka la Bulk, Steven Mollel, aliwashukuru watoa huduma hao kwa huduma bora waliyopewa kwa wakati,  pia aliwasihi wananchi wengine kwenda kununua bidhaa za Bulk akibainisha

“Vifaa vyao vina ubora wa hali ya juu, Ninawahimiza wananchi wote wajitokeze kununua hapa ili miradi yao ya ujenzi iweze kufanyika kwa ubora,” alisema Mollel.


 

Wateja wanahimizwa kutembelea maduka ya Bulk ili kunufaika na punguzo hili, huku kila siku wakiwa na nafasi ya kushinda jiko poa litakalopewa kwa bahati nasibu.




Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yanalenga kuimarisha uhusiano kati ya watoa huduma na wateja, kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya biashara, na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna bora ya kutumia bidhaa na huduma zinazopatikana nchini.

Bulk, kwa kauli mbiu yake “Less Shillings, More Value”, inabaki kuwa taasisi ya kuaminika na yenye mchango mkubwa katika kuendeleza ubora wa vifaa vya ujenzi na huduma kwa wateja, ikiweka mfano wa kampuni inayowajali wateja wake na jamii kwa ujumla.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia