MANYARA: WACHIMBAJI WA MADINI WAUNGANA KUMPONGEZA RAIS SAMIA, WAHIMIZA UTULIVU WA NCHI




Na Woinde Shizza, Manyara

Mwenyekiti wa wachimbaji wa madini mkoa wa Manyara, Elisha Nelson, amewataka wananchi wa Tanzania kulinda amani ya nchi, hususani katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi wa kitaifa.

Amesema hayo alipouzuria katika mahafali ya tano ya Shule ya Glisten Pre and Primary School, iliyopo Mererani, Manyara, huku akisisitiza umuhimu wa wazazi, walimu na wanafunzi kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii.

Nelson alisisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya October 29, akisisitiza kuwa kila kura ni nyenzo muhimu ya kuchagua viongozi wa maendeleo.

Aidha, Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa uchaguzi ni fursa ya wananchi kuchagua Rais, madiwani na wabunge wanaoweza kuleta maendeleo ya kweli kwenye taifa.

Pia, alitoa wito maalumu kwa wachimbaji wote wa madini kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi, akisisitiza kuwa kupiga kura ni kutimiza haki yao ya msingi.

Aliongeza kuwa amani na mshikamano wa kijamii ni msingi wa taifa lenye maendeleo, na kila Mtanzania anapaswa kuchukua jukumu lake kwa uzito.

Nelson aliwataka wananchi Wote kumuunga mkono Rais Samia na viongozi wa CCM kwani hii ni njia ya kuhakikisha maendeleo endelevu katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

“Tuendelee kulinda umoja na amani yetu, na tujitokeze kwa wingi kupiga kura, hii ndiyo njia ya kuhakikisha maendeleo ya taifa letu yanatimia,” alimalizia, huku akishirikiana na shule kusherehekea mafanikio ya wanafunzi.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia