WAZAZI WAKARIBISHWA KUANDIKISHA WATOTO KWA ELIMU BORA




WAZAZI WAKARIBISHWA KUANDIKISHA WATOTO KWA ELIMU BORA

Munyuku: Tunawaandaa watoto kitaaluma na kivitendo kwa maisha ya baadaye


Mwalimu mkuu wa Arusha Integrated School, Rems Munyuku, amesema shule hiyo ya awali na msingi imeendelea kutoa elimu bora yenye ubora wa hali ya juu na malezi yenye nidhamu, jambo linaloifanya kuwa chaguo sahihi kwa wazazi wanaotafuta elimu yenye matokeo chanya.

Akizungumza katika mahafali ya 14 ya shule hiyo yaliyofanyika jijini Arusha, Munyuku alisema jumla ya wanafunzi 18 wamehitimu mwaka huu, wakiwa wameandaliwa kitaaluma na kimaadili kwa hatua zinazofuata, huku wakifundishwa pia elimu ya vitendo itakayowasaidia hata kujitegemea.

Aidha, alibainisha kuwa wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo wamekuwa wakifanya vizuri kwa kupata alama A kwenye mitihani yao ya taifa, na kuongeza kuwa anaamini hata wahitimu wa mwaka huu wataendeleza historia hiyo ya mafanikio.

Alisema shule hiyo inapokea watoto kuanzia elimu ya awali wakiwa na umri wa miaka miwili hadi darasa la saba, sambamba na madarasa ya kuhamia kwa wanafunzi kutoka shule nyingine.

Kwa mujibu wa Munyuku, faida kubwa za kujiunga na shule hiyo ni pamoja na ubora wa elimu unaotolewa na walimu wenye uzoefu, elimu ya vitendo inayomwezesha mwanafunzi kujitegemea, mazingira salama kwa watoto, malezi yenye nidhamu na maadili bora pamoja na nafasi za kuandikisha watoto kuanzia elimu ya awali, msingi na madarasa ya kuhamia.



Tunaamini kila mtoto anastahili kupata elimu bora. Tunawakaribisha wazazi kuleta watoto wao kwani shule yetu imejipanga kumwandaa mtoto kitaaluma, kimaadili na kivitendo kwa maisha ya baadaye,” alisema Munyuku.


About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia