WAFANYAKAZI
wa kampuni ya uwakala wa kukusanya ushuru wa maegesho ya magari jijini Arusha ya
Kilimanjaro Printers(KPL) wameiingiza katika kashfa nzito kampuni hiyo baada ya
kutuhumiwa kusababisha upotevu(kuiba) wa fedha za kigeni za watalii wa Kirusi
kiasi cha dola 55,000.
Upotevu
huo unadaiwa kutokana na wafanyakazi wa kampuni hiyo kubeba gari la kitalii lililokua
na fedha hizo bila ya dereva wake kuwepo ndani ya gari alipokua ameliegesha.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya utalii
ya Africa Smart Safari inayodai fedha hizo ambae ndiye mmiliki wa gari hilo lenye
namba za usajili T302ABB Toyota Spacio,Sotet Mutambalike alisema gari yake
ilichukuliwa kibabe na wafanyakazi wa KPL eneo la kituo cha mafuta cha Five
Star kilichopo eneo la Unga ltd akijianda kupeleka fedha hizo benki.
Mutambalike
alisema fedha hizo za kigeni ni malipo ya makundi manne ya watalii wa Kirusi
waliokuwa wakitaka kutumia kampuni hiyo kwenda kupanda mlima Kilimanjaro.
Akieleza
mkasa mzima kwa waandishi wa habari alisema aliwahi kufuatwa na
mfanyakazi wa KPL eneo la karibu na stand ndogo ya magari ya usafiri wa Jiji la
Arusha{Vifodi} juu ya ushuru wa gari ya sh, 200/= na alitoa noti ya shilingi
10,000 lakini mfanyakazi huyo hakuwa na chechi ya kurudisha.
Alisema
baada ya mfanyakazi huyo kukosa cheNchi ya shilingi 10,00 alimpa noti nyingine
ya shilingi 5,000 ambayo nayo alikosa chenchi yake na ndipo alipomwambia kuwa
anakwenda uwanja wa ndege kupeleka wageni na akirudi angempatia pesa yake.
Mkurugenzi
huyo aliendelea kusema kuwa juzi akiwa na gari ndogo iliyokamatwa alipigiwa
simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Lewis ambaye baadae aligundua
kuwa ni meneja wa KPL kuwa alikuwa akimtafuata na walikubaliana kukutana eneo
gari lilikokamatwa.
‘’Meneja
huyo alikuja eneo nilikokuwa nimegesha gari nikijiandaa kwenda kula ghafla
aliniita chemba lakini cha kushangaza niliona wafanyakazi wake wakibeba gari
yangu na niliwaambia kuwa humo ndani kuna fedha ngoja nitoe
sikusikilizwa’’alisema
Alisema
baada kuchukuliwa gari hilo aliripoti katika ofisi ya mwanasheria wa Jiji
la Arusha na ofisi hiyo iliuagiza uongozi wa kampuni ya KPL kutoa gari hilo
kwani kosa ni la wafanyakazi wa kampuni yao ya kukusanya ushuru kwa
kutokuwa na chechi za kurudisha lakini walikaidi amri hiyo.
Mutambalike
alisema baada ya kuona hali hiyo aliripoti kituo cha kati cha polisi na
kufungua faili lenye namba RB/13441/2012 juu upotevu wa fedha hizo na polisi
ilikuwa ikiwasaka watuhumiwa wa kampuni ya KPL.
Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alikiri kuripotiwa kwa tukio hilo kituoni hapo na
kudai kuwa linafanyiwa uchunguzi na ikibainika kuwa sheria na taratibu
zilikiukwa wahusika wote watachukuliwa hatua.
“hilo tukio la upotevu wa
dola lipo na tunalifanyia kazi na wahusika walijaribu kukiuka taratibu
wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria’’alisema kamanda Sabas.
Naye
Meneja huyo wa KPL Edward Lewis alipopigiwa simu alikiri gari hilo
kushikiliwa na kampuni hiyo na kueleza kuwa mmiliki wa gari hilo hakutoa ushirikiano wowote.
Lewis
alisema gari yao aina ya break Down yenye namba
za usajili T61ADB ndio iliyovuta gari hilo
na kupeleka ndani ya viwanja wa shirika la usagaji la Taifa{NMC}.
Meneja
huyo alisema kuwa hawezi kujua kama ndani ya gari hilo
kulikuwa na dola kwani yeye hakufanya kazi ya kulibeba gari hilo.