BREAKING NEWS

Tuesday, September 6, 2016

WAFANYAKAZI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WATINGA MAHAKAMANI



Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat
Mfumukeko.

Na Woinde shizza,Arusha

Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
wamefungua kesi kumshtaki Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo
kwa madai ya kuvunja mikataba ya ajira.

Kesi hiyo wameifungua katika Mahakama ya Haki ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EACJ) kitengo cha awali.

Wafanyakazi watatu kutoka Idara ya Amani na Usalama
wanadai Juni 17, Katibu Mkuu huyo alivunja mikataba yao ya
ajira kinyume na agizo la Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki waliyoyatoa kwenye mkutano wa nyongeza
wa 31 na kwa kuzingatia Kanuni ya 96 ya taratibu za
wafanyakazi wa EAC ya mwaka 2006.

Wanadai kuwa walipokea barua kutoka Masjala ya EAC yenye
notisi ya miezi mitatu ya kusitishwa kwa ajira zao iliyowekwa
saini na katibu mkuu huyo, huku ikieleza kuwa EAC haina
fedha za kuendeleza mradi wa APSA unaopata fungu kutoka
Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Umoja wa Afrika (AU).


Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates