Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO),Dkt Richard Banda aliyesimama, akizungumza wakati wa kukabidhi dawa za kutibu maji, wa kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwangilia Injinia Mbogo Mfutakamba,na wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya StephanoKiberiti na wa mwisho kulia ni Mkurungezi Msaidizi TAMISEMI Eng.Enock Nyanda.
Katibu Mkuu Mfutakamba akitia saini baada ya makabidhiano ya Dawa hizo za kutibu maji,huku zoezi hilo likishuhidiwa na Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO),Dkt Richard Banda na Mkurungezi Msaidizi TAMISEMI Eng.Enock Nyanda.
Katibu Mkuu Mfutakamba wa kulia akibadilishana hati za makabidhiano na Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO),Dkt Richard Banda.
Na Sheila Simba,Maelezo.
Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwangiliaji, imepokea mchango wa dawa za kutibu maji aina ya (calcium hypochlorite) kiasi cha kilogramu 49,500 kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zitakazo sambazwa kwa mamlaka ndogo za maji nchini.
Akipokea dawa hizo leo Jijini Dar Es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia Mbogo Mfutakamba, alisema kuwa dawa hizo zitasambazwa kwenye Halmashauri mbalimbali kama mchango wa shirika hilo katika kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama.
“Naziagiza Halmashauri na Mamlaka za maji kote nchini ambazo zimeainishwa kupatiwa dwa hizo kuzitumia kwa usahihi ili kukidhi lengo lililokusudiwa”alisema
Ameeleza kuwa serikali imejiwekea malengo ifikapo mwaka 2020 kuhakikisha asilimia 85 wananchi wanaoishi vijijini wanapata majisafi na salama na asilimia 90 ya wananchi waishio mijini wanapata huduma hiyo muhimu.
Amesema kuwa dawa hizo zitasambazwa kutokana na uhitaji wa maji katika eneo husika na kutoa mfano wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga ambayo imepata mapipa sitini kutokana na kuzalisha maji mengi.
“Serikali itaendelea kuchangia katika mamlaka za maji ili kuwapatia watu majisafi ili kuondoka na tatizo la kipindupindu katika baadhi ya maeneo”alisema Mfutakamba
Akitoa shukurani kwa niaba ya Serikali ya Tanzania Katibu Mkuu huyo Injia Mfutakamba,amesema kuwa WHO ni shirika la mfano wa kuigwa na wadau wengine kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwapitia wananchi majisafi na salama.
Kwa upande wake mwakilishi wa (WHO) Dkt Richard Banda alisema kuwa dawa hizo zitasaidia katika kusafisha maji na ili kusaidia jamii kupata maji safi ya kunywa.
“WHO tutaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutokomeza,magonjwa yanayosababishwa na utumiaji wa maji ambayo sio salama”alisema Banda.