Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa utambuzi na usajili
wakazi waishio Wilayani hum
Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji Kata, Waratibu elimu Kata, na Maafisa kilimo ngazi ya Tarafa wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa utambuzi na usajili
wakazi waishio Wilayani humo
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Bw Dandala Mzunguor akiwatambulisho waratibu kutoka Nida kwa ajili ya kutoa elimu ya namna ya kuendesha zoezi la utambuzi na usajili kwa wakazi
Kaimu Mkurugezni wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Haika Massawe akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa Mradi huo unasimamiwa na Nida
Na
Mathias Canal, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amezindua Mradi wa utambuzi na usajili
wakazi waishio Wilayani humo wenye umri wa miaka 18 na zaidi ili kuhakikisha
taarifa zao zinatambulika kitaifa na kimataifa ambapo Mamlaka ya vitambulisho
vya Taifa NIDA ndio wasimamizi wa zoezi hilo.
Akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji
Kata, Waratibu elimu Kata, na Maafisa Kilimo wa ngazi ya Tarafa, Dc Mtaturu
amesema kuwa Mradi huo utasaidia serikali kutambua wakazi wake wenye umri wa
kuanzia umri wa miaka 18 ili kuainisha namna bora ya kuwawezesha vijana kupitia
vikundi sambamba na umri wa zaidi ya miaka hiyo.
Mtaturu pia amewataka watendaji kusimamia vyema
mapato ya serikali na kutoa risiti kwa kila malipo yanayofanyika ili ili
kuepusha usumbufu kwa wananchi ambao wana jitahidi kwenda na kasi ya serikali
ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli lakini wanakwamishwa na
baadhi ya watendaji.
Hata hivyo aliwataka watendaji hao kumaliza haraka
matatizo ya wananchi ambayo yamekomaa na hatimaye kuwa sugu kwani wasipofanya hivyo ni kukwepa majukumu yao
hivyo kukosa siafa ya kuwa watumishi wa serikali kwani bado wana mtazamo hasi
kwa kufanya kazi kwa mazoea.
Majukumu mahususi ya NIDA ni kutoa vitambulisho kwa
Watanzania na wageni wakazi wa Tanzania na kutunza daftari la Utambuzi kwa
lengo la kuimarisha usalama na amani, Kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya
Taifa.
Dc Mtaturu alisema Mradi huo unatarajia hadi kufikia
Disemba 31, 2016 usajili uwe umekamilika nchi nzima na kutoa namba ya
utambulisho (NIN) kwa waombaji wote wenye sifa za kupewa kitambulisho vya Uraia.
Msimamizi Mkuu wa Mradi huo Agnes Mtei amesema kuwa
miongoni mwa matarijo ya mradi huo ni pamoja na kuanza rasmi kwa matumizi ya
vitambulisho vya Taifa katika upatikanaji wa huduma mbalimbali, kuboreshwa kwa
huduma za jamii hususani upatikanaji wa huduma kwa haraka hasa zile
zinazohitaji utambulisho na uhakiki, Upatikanaji wa taarifa kwa haraka na
kupunguza ukiritimba katika upatikanaji wa huduma, Kuongeza wigo wa ukusanyaji
mapato (Kodi) pamoja na kuongeza idadi ya walipa kodi na Kuunganika kwa mifumo
mbalimbaliya serikali na binafsi na hivyo kuongeza matumizi ya huduma kwa mfumo
wa kielektroniki.
Mtei alisema kuwa katika kukamilisha zoezi hilo ni
lazima kwa kila mwananchi, mgeni na mkimbizi anayeishi kihalali kujaza fomu ya
maombi ya Vitambulisho ambapo kwa wale ambao hawana uwezo wa kujaza fomu hizo
kwa sababu mbalimbali wanaruhusiwa kujaza/kujaziwa fomu hizo lakini lazima
wathibitishe kuwa taarifa zilizojazwa ni za kwake na sahihi.
Mfumo wa usajili na utambuzi wa watu ni mfumo
unaotambulika kwa chachu ya kukua kwa haraka kwa maendeleo ya kiuchumi duniani
ambapo unatambulika kama mfumo wa kipekee katika mapambano dhidi ya vitendo vya
kigaidi na mfumo utakao saidia kusukuma mbele mabadiliko ya haraka katika
maendeleo ya nchi na mtu mmoja mmoja hivyo kutokana na jambo hilo serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ikaamua kuanzisha mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
NIDA Agosti 01 Mwaka 2008.