Waandishi wa Habari kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu, wakiwa kwenye semina iliyofanyika Jumamosi wiki iliyopita Septemba 23, 2016 Jijini Dar es salaam.
Semina hiyo iliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA, ambapo pamoja na mambo mengine iliangazia kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari kuhusu mafanikio na changamo za wanawake ili kufanya jamii iwatambue na hivyo kuwafunguliwa fursa mpya ikiwemo kujitokeza kwenye masuala ya uongozi.
Na BMG
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA, Alakok Mayombo, akifungua semina hiyo.
Kushoto ni mkufunzi katika semina hiyo, Valerie Msoka ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya InterNews tawi la Tanzania. Pia ni Mkurugenzi mstaafu wa TAMWA.
Godfrida Jola ambaye ni Afisa Miradi TAMWA, akizungumza jambo kwenye semina hiyo
Mshiriki
Mshiriki kutoka Kanda ya Ziwa
Mshiriki
Mmoja wa wanasemina
Wanasemina
Mmoja wa wanasemina akichangia jambo
Wanasemina kwenye majadiliano
Wanasemina kwenye majadiliano
Wanasemina kwenye majadiliano
Makabidhiano ya nakala mbalimbali kutoka TAMWA
Kulia ni Godfrida Jola kutoka TAMWA na kushoto ni George Binagi-GB Pazzo kutoka Lake Fm Mwanza & BMG.
*****************************************
Vyombo vya habari nchini vimehimizwa kutoa fursa kwa
wanawake kuonesha umahiri wa utendaji wao wa kazi ili kuleta chachu kwa
wanawake wengi zaidi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania TAMWA, Alakok Mayombo, alitoa
rai hiyo jumamosi iliyopita kwenye mafunzo kwa wanaandishi wa habari kutoka
mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu yaliyofanyika jijini dar es salaam.
Alisema bado idadi ya wanawake walio kwenye nafasi
mbalimbali za uongozi serikalini ni chini ya asilimia 30 kwa nchi za kusini mwa
Bara la Afrika ikiwemo Tanzania hivyo waandishi wa habari wana nafasi kubwa
kuwahamasisha wanawake kujitokeza kuwania nafasi za uongozi.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo
ambayo yaliandaliwa na TAMWA, walisema mafunzo hayo yawatawasaidia kuandaa
vipindi bora vitakavyowahamasisha wanawake nchini kujitokea kuwania nafasi za
uongozi katika jamii.
Soma HAPA Mafunzo ya Kanda ya Ziwa