Bw Donsun Lee ambaye ni
Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International akikagua pump kwenye
moja ya kisima kwenye shule ya Msingi Makalala, anayetizama ni Mbunge wa
Mafinga Mjini Cosato Chumi
Bw Donsun Lee ambaye ni
Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International akimsikiliza
kwa makini Mhandisi wa Maji wa Mji wa Mafinga Eng Eradius.
Pichani baadhi ya wanafunzi
na waalimu wa shule ya Msingi Makalala wakiwa katika picha ya pamoja na Mrs Lee
na Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi
na fredy mgunda,iringa
MBUNGE wa jimbo Mafinga
mjini Cosato Chumi ameendeleza juhudi zake za kuwatafutia maendeleo wananchi wa
jimbo lake kwa kufanya kazi kwa ukaribu na taasisi za kiserikali na zisizo za
kiserikali za nje ya nchi ya Tanzania pamoja na taasisi za ndani.
Hivi karibu balozi wa korea
nchini Tanzania Bw Song Geum Young akiwa na NGO ya Kutoka Korea ya World share alitembelea jimbo la mafinga mjini kwa lengo la kujionea
changamoto za jimbo hilo na kutafuta njia za kutoa msaada wa kutatua baadhi ya
changamoto hizo na walitoa msaada wa taa ndogo za solar kwa kaya masiki mia saba.
Baada ya balozi huyo kurudi
jijini Dar es Salaam alimuagiza Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving
Friends International Bw Donsun Lee kutembelea jimbo la mafinga mjini na
kuzifanyia tafiti kwa kina baadhi ya changamoto za jimbo hilo ambazo alikuwa
amezianisha hapo awali ili kuweza kusaidia kuzitatua.
Aidha mkurugenzi wa NGO ya
Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee
alifanikiwa kutembelea baadhi ya shule za jimbo la mafinga mjini na kuzifanyia
tafiti changamoto zilizopo kama uhaba wa maji na kuahidi kuzitatua kwa kuwa
ameshazifanyia utafiti.
“Leo nimetembelea Shule za
Msingi Makalala, Mkombwe, Ndolezi na Mwongozo na Shule ya Sekondari Luganga na
nimejionea shida ya upatikanaji wa maji hivyo kwa kuwa NGO yetu inajihusisha
na uchimbaji wa visima hivyo tumewasilisha taarifa hizi makao makuu ya ofisi zetu na tunasubili majibu”alisema Bw Donsun Lee.
Bw Donsun Lee alimpongeza mbunge wa jimbo mafinga mjini Cosato Chumi kwa juhudi alizozifanya za
kuwashawishi kutembelea jimbo hilo na kujionea baadhi ya changamoto ambazo
wanaweza kuzitatua kwa kushiriana na mbunge huyo.
Katika ziara hiyo Bw Lee na
timu yake walitembelea Shule za Msingi Makalala, Mkombwe, Ndolezi na Mwongozo
na Shule ya Sekondari Luganga.
Aidha baada ya tafiti hizo,
Bw Lee atawasilisha taarifa zake Makao Makuu ya NGO ya Serving Friends
International huko Seoul, Korea.
Nia ya kufanya tafiti hizo
ni kuiweka Katika Mipango Halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa sababu ndo
utaratibu wa NGO hiyo ambayo kwa Sasa wanachimba visima mkoani Singida
Kwa upande wake mbunge wa
jimbo la mafinga Cosato Chumi amemshukuru Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya
Serving Friends International Bw Donsun Lee kwa kufanikisha kufanya tafiti
ambazo amejine mwenye na kuleta matumaini kwa wananchi wa jimbo hilo la kutatuliwa
tatizo la maji kwa kuchimbiwa visima na taasisi hiyo.
Chumi ameongeza kuwa haya ni
matokeo ya ziara ya Balozi wa Korea ambaye alitembelea jimbo la Mafinga Mwezi
mmoja uliopita na kujionea changamoto hizo.
Lakini mbunge Chumi
amewataka wananchi wa jimbo la mafinga kufanya kazi kwa kujituma na kuunganisha
na nguvu za mbunge wao ili kupata maendeleo kwa kasi inayotakiwa.
“Unakuta mbunge nahangaika
kuwaletea maendeleo wananchi wangu kama hivi mnavyoona lakini ukienda vijiweni
unakuta wananchi wanacheza bao,pooltable na wengi wanapiga soga zisizo na
malengo,wakati wangeutumia muda huo kufanya kazi jimbo la mafinga mjini
litakuwa na maendeleo ya kasi sio muda”.alisema Chumi