Na Mathias Canal, Dodoma
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya wananchi (FDC)-CHISALU amekalia kuti kavu
mara baada ya kubainika kuwa ameruhusu udahili wa wanafunzi wanaosoma
fani ya utaalamu wa Kilimo na Mifugo ilihali chuo hicho ni maalumu kwa
ajili ya mafunzo ya utaalamu wa Maendeleo ya jamii (Community
Development).
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri
amemsimamisha kazi Mkuu huyo kutokana na kupokea malalamiko ya baadhi ya
wanafunzi chuoni hapo ambapo malalaniko yao yamekuwa na hoja za msingi
zilizopelekea kuibuka kwa kadhia mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho.
Katika kutaka kubaini udhaifu unaohusu utendaji wa uongozi wa chuo
hicho Dc Shekimweri alisikiliza hoja za wanafunzi chuoni hapo ambapo
walitaka kujua sababu zinazopelekea wao kufanya mtihani unaoandaliwa na
Chuo cha Ufundi VETA ilihali mtaala wao sio wa VETA.
Mbali na
kadhia hiyo wanafunzi hao wamehoji pia fani ya kilimo wanafunzi hao
wanayosoma ya Kilimo na Mifugo ambayo haitakiwi kwa mujibu wa taratibu
pia haina namba ya mtihani (Exam Code) hivyo ni kwa kiasi gani wanafunzi
hao watahakikishiwa ajira kama maafisa Mifugo pindi wamalizapo masomo
yao.
Dc Shekimweri alizuru Chuoni hapo kwa lengo la kutaka kujua
hatma ya wanafunzi wa chuo hicho kufungwa pasina sababu ndipo alipobaini
uongo uliotumiwa na Mkuu wa Chuo hicho kwa kudai kuwa chuo kimefungwa
kwa sababu ya kujiandaa na mitihani ambapo hata hivyo mtihani huo
unataraji kufanyika Oktoba 10, 2016.
Mkuu wa chuo hicho alieleza
kuwa chuo hicho kitafungwa hadi Tarehe 9/10/2016 siku moja kabla ya
kufanyika kwa mitihani ambapo janja hiyo ilibainiwa na Mkuu wa Chuo kwa
kudanganywa ratiba ya mtihani huo ambayo inaonyesha kuwa tarehe
26/09/2016 ndipo ambapo mtihani huo unataraji kuanza.
Hata hivyo
Mkuu huyo wa chuo hicho amefunga chuo hicho pasina kushirikisha Bodi ya
Chuo ambapo pia alihoji sababu za kudanganywa kufungwa chuo hicho bila
maamuzi ya kusitisha kufanyika kwa mitihani ambapo ratiba yake imekwisha
tolewa jambo ambalo lilimuacha mdomo wazi Mkuu huyo wa Chuo hicho.
Kutokana na kadhia hizo Dc Shekimweri amemsimamisha kazi Mkuu wa chuo
hicho kwa kutumia uongo wakati wa kujitetea na kushindwa kitekeleza
majukumu yake kikamilifu ikiwemo kutoitisha vikao vya Bodi, Kutosikiliza
kero za wanafunzi hata alipojulishwa kwa maandishi na wanafunzi hao,
kufunga chuo kwa dharula ilihali tatiba ya mtihani inaendelea na
kuwashauri vibaya wanafunzi kuhusu hatima yao kutokana na mkanganyiko wa
mtaala.
Dc Shekimweri alisema kuwa serikali hii ya awamu ya tano
chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inahubiri zaidi uwajibikaji hivyo
maamuzi hayo yanatuma salamu ili mamlaka ya uteuzi ifuatilie na
kushughulikia tuhuma dhidi yake na kuchukua stahiki za kisheria.
Mkuu huyo wa Wilaya amesitisha Bodi ya chuo na kumtaka mwenye mamlaka
nanuteuzi wa Bodi aivunje Bodi hiyo kwa kushindwa kukutana hata mara
moja tangu bodi hiyo ilipoanzishwa Mwaka 2013hivyo kushindwa kitafsiri
na kusimamia Dira kwenye mpango mkakati (Strategic Plan) pia kutokuwa na
kalenda ya mwaka wa taaluma.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya pia
alihoji pasina kupatiwa majibu kuhusu uidhinishwaji wa mpango wa bajeti
wa chuo kuhusu anayeufanya ilihali Bodi haikutani kwa ajili ya vikao.
Dc Shekimweri alienda mbali zaidi kwa kutaka kujua vipi vipaombele vya
chuo, mabadilko na mitaala, mafanikio na changamoto za chuo vinajadiliwa
na kufikiwa maamuzi na watu gani iwapo Bodi haikutani kujadili.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya ya Mpwapwa alisema Changamoto za mitaala,
Udahili na mtihani pamoja na vyeti vya kuhitimu litafanyiwa kazi kwenye
Mamlaka husika (VETA) na Wizara ya Maendeleo ya Jamii.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia