Na Woinde Shizza,Arusha.
Wajasiriamali
nchini wametakiwa kujikita katika Ufugaji wa kuku wa Kienyeji na kisasa ili
waweze kunufaika kiuchumi kufuatia ongezeko la uhitaji mkubwa wa mayai na nyama
katika maeneo ya mengi hususan kwa wafanyabiashara wa vyakula.
Hayo
yameelezwa na Mjasiriamali Boniventura Shiyo anayejihusisha na ufugaji huo
amesema kuwa kwa sasa biashara hiyo imemuongezea kipato ambacho anakitumia
kujiletea maendeleo pamoja na kuendesha familia pasipo kuyumba.
Mjasiriamali
huyo amewataka Watanzania kujenga tabia ya uthubutu kwani soko la biashara ya
kuku ni kubwa na linazidi kukua kila kukicha.
Hata hivyo
Boniventura amesema kuwa kwa sasa anatumuia mashine maalumu ya inayototoa mayai
na kuwa vifaranga maarufu kama incubator ambayo imemuongezea fursa ya kuwa
muuzaji wa vifaranga pia.
Biashara ya
ufugaji wa kuku ni moja kati ya biashara zinazoshamiri kwa kasi katika maeneo
mingi nchini hususan maeneo ya mijini ambapo ndipo masoko makubwa yanapatikana
kutokana na idadi kubwa ya watumiaji wa bidhaa za mayai na nyama ya kuku.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia