WAfanyakazi wakiwa kazini kuratibu shughuli hiyo ya maboresho ya rasimu ya huduma kwa mteja
Mamlaka ya
maji safi na usafi wa mazingiza imewataka wakazi wa jiji la Arusha kukaa mkao
wa kula kwani wapo katika wakati wa kuboresha huduma zake kwenye kipindi cha
miaka miwili na nusu iliyobakia katika uboresha wa miundombinu na utafutaji wa
vyanzo vipya vya maji na kuwa tatizo la maji litakuwa historia.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkurugenzi wa AUWSA Ruth Koya wakati akijibu maswali ya wadau
mbali mbali walioshiriki kwenye Mkutano wa maboresho ya mkataba wa huduma kwa
wateja jijini Arusha.
Alisema kuwa
kumekuwa na matatizo ya upungufu wa maji kwa mda mrefu na serikali imeliona
hilo ndio maana ikatenga kiasi cha tsh,476 bilion za uboreshaji wa huduma mbali
mbali za mamlaka hiyo hivyo suala hilo linafanyiwa kazi kuanzia mwaka huu hadi
mwaka 2018 litakapokamilika.
“Tuwe na
subra maradi huu kwa sasa una mda wa miezi nane tangia uanze na mkandarasi wa
utafutaji wa vyanzo vya maji yupo kazi akishakamilisha tutaanza maboresho ya
miundombinu yetu ilkuweza kuwafikishia maji kwa wateja wetu wote”alisema Koya
Kwa upande
wake kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Arusha Afisa tarafa wa jiji la Arusha
Felician Rutehengerwa aliitaka Auwsa kuwabainisha wezi wote wa maji ilikuweza
kuwafisha katika mikono ya kisheria kwani suala hilo pia linachangia wananchi
kukosa huduma ya maji safi na upotevu wa maji.
Alisema kuwa
kumekuwapo na vyanzo vingi vya maji zaidi ya 19 na vingine vimeanzishwa na
viwanda ambavyo vimekuwa vikiikosesha Auwsa mapato ikiwemo kiwanda cha A to Z ambacho kimekuwa kikigawa maji bure
huku wakitambua kuwa wao hawana mamlaka ya kisheria ya usimamizi wa maji hivyo
ni mteja mkubwa mnampoteza kulipa huduma za maji.
Nae
Mwenyekiti wa Bodi ya Auwsa Job Laizer alisema kuwa Malalamiko ambayo wananchi
wameyatoa ni changamoto kubwa kwao katika kuifanya mamlaka hiyo kuboresha
huduma zake na kuwaahidi wadau kuyasimamia na kuahkikisha wateja wanapata
huduma bora na kwa wakati.
|
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia