Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupewa dhamana
mwenyekiti wa UVCCM akiwa anatoka mahakamani mara baada yakupewa dhamana
Na Woinde Shizza,Arusha
Mahakama
ya Hakimu mkazi Arusha imemsomea
mashtaka mawili Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya ambaye
pia ni diwani wa kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini .
Miongoni
mwa makosa hayo aliyosomewa mahakamani hapo kosa la kwanza alituhumiwa kujifanya Afisa mtumishi wa serekali (TISS)huku
kosa la pili ikiwa kugushi moja ya nyaraka za serekali(kitambulisho ).
Akisoma
mashtaka hayo mahakamani hapo Wakili wa
serekali Lilian Mmasi alisema kuwa Mnamo
May 18 katika hotel ya Skyway
iliopo makao mapya jijini Arusha Mshitakiwa alijitambulisha kama Afisa
utumishi wa idara ya usalama wa taifa na kufanya Utapeli .
Wakili
Mmasi alitaja kosa la pili ambalo Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya alisomewa kuwa
ni kugushi kitambulisho cha idara ya usalama wa Taifa kilichokuwa kikisomeka jamuhuri ya muungano
wa Tanzania idara ya usalama wa Taifa (TISS) Lengai Ole Sabaya kikosi maalumu
Agent (undercover)chenye code no MT 86117 huku akitambua kuwa ni kinyume cha kisheria .
Hata hivyo mara baada ya kusomewa mashtaka hayo
mahakamani hapo mtuhumiwa alikana mashtaka ndipo Hakimu Mkazi aliyekuwa
akisikiliza kesi hiyo Gwantwa Mwamkuga
Alisema dhamana ipo wazi iwapo wathamini watakithi vigezo vinavyotakiwa na
mahakama hiyo.
Hata
hivyo Mshitakiwa alipata dhamana baada ya kukithi vigezo vilivyowekwa na
mahakama ambapo ilikuwa ni wadhamini wawili wenye sifa ambapo kwanza awe
mtumishi wa serikali pili awe na mali
isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa kila mmoja.
Kesi imeairishwa na hakimu mkazi hadi itapotajwa tena October 5 ambapo uchunguzi unatarajiwa kukamilika na
kesi hiyo kuanza kusikilizwa.
Mara
baada yakupata dhamana mahakamani hapo
wakili wa mtuhumiwa Yoyo Asubui alisema kuwa mshtakiwa amesomewa
mashtaka yote mawili na kukana mashtaka ambapo wanatarajia uchunguzi
ukikamilika kesi itaanza kusikilizwa
mapema na haki kutendeka ,huku akimtaka mteja wake kuendelea na majukumu ya
mandeleo kwa wananchi wa kata ya Sambasha.
“kwakweli
kesi hii sio ya kweli na naweza kusema ipo kisiasa na nashukuru jeshi la polisi kwa kunishikilia na kukaa na
mimi vyema hadi kunileta mahakamani ambapo naamini haki itatendeka na ukweli
utabainika “Alisema Sabaya mara baada ya kupata dhamana
Alisema
kuwa hili limetokea mara baada ya kuwatoa wabadhilifu wa mali za umoja wa
vijana (UVCCM) ambapo kwa muda mrefu wamekuw a mali za umoja huo kujinufaisha
wenyewe na vijana kukosa maendeleo kupitia miradi ya umoja huo.