Na Sheila Simba-Dar es salaam.
Wapenda
amani nchini wamelaani kitendo cha Jukwaa la Wahariri (TEF)kutoa tamko dhidi
Serikali kuhusu kufungia vituo viwili vya redio hivi karibuni.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti Jijini Dar es Salaam, wameonyesha Dhahiri kuchukizwa na TEF
na kusema hawajui wanalolifanya.
Bwana
Juma Ramadhan, Mkazi wa Ilala, amesema kuwa hapendezwi na watu kutetea chombo
kinachohatarisha amani Nchi na mali zao kwa kuandika habari za uchochezi.
“Mimi
nimekaa nchini kwa kipindi kirefu sijaona machafuko je huyu anayechochea
uvunjifu wa amani ana lengo gani kwa Taifa?”, aliuliza Ramadhani
Naye
Bi Mercy Mwakitalima Mkazi wa Sinza,
amesema kuwa Jukwaa hilo linapaswa kusimamia na kuongoza vyombo wanavyosimamia
kutokutumia maneno na lugha isiyofaa ili kuepeka kuliingiza taifa katika
machafuko.
Ameongeza
kuwa wahariri wanapaswa kusimamia maadili ya uandishi wa habari ili vyombo vyao
viandike habari zinazingatia umoja kitaifa uliojengeka kwa muda mrefu.
“Taifa
letu ni la amani na inatakiwa kulindwa kwa gharama yoyote,naviomba vyombo vya
habari nchini kuheshimu sheria za Nchi,ki ukweli siku hizi baadhi ya vyombo
wanaongea sana vitu ambavyo havina faida yoyote kwa jamii, naipongeza Serikali
kwa hatua waliochukua ili iwe fundisho kwa wengine”alisema Mwakitalima
Ameongeza
kuwa sekta ya habari nchini inatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhubiri
amani na sio kutumia maneno yanayochochea uvunjifu wa amani kwani kufanya hivyo
kutapelekea Taifa pabaya kwa kuwalisha watanzania vitu visivyofaa.
Kwa
upande Mwalimu wa shule ya Msingi Kinondoni aliyejitambulisha kwa jina moja la
Mwamvua,ameiomba Serikali kuharakisha Muswada habari ili kuwa na watu wenye
sifa pekee katika sekta ya habari kwani kwasasa sekta ya habari imepoteza
umaarufu wake.
“sekta
ya habari nchini kwa sasa haina mwelekeo kila mtu ni mwandishi wa habari bila
hata kuwa na taaluma ya habari hili ni tatizo lazima Serikali ilifanyie kazi
mapema ili kuepeuka kuwa na watu wasiojua maadili ya kazi hiyo,”alisema Mwamvua.
Naye
Joseph Jeremia ameomba Serikali kuendelea kuvichukulia hatua vyombo vya habari
ambavyo vinamwelekeo wa kuhatarisha amani ya Tanzania kwa kuvifuta kabisa.
Amesema
amani ni rahisi kuipoteza lakini ni kazi ngumu kuijenga kama ilivyo hapa
nchini.
Jukwaa
la wahariri walitoa tamko hilo, kufutia Serikali kupitia kwa Waziri wa
Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Nape Nnauye, kutangaza kufungia vituo viwili
vya radio kwa kutangaza habari za uchochezi,ambazo ni Radio five ya Arusha na
Radio Magic fm ya jijini Dar es salaam.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia