Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo amewataka viongozi wa dini
nchini kuwa waaaminifu kwenye matumizi ya fedha wanazopatiwa na wahisani
kwa lengo la kusaidia jamii ya watanzania ambao ndiyo walengwa wa misaada
hiyo.
Mhe Jaffo ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam kwenye mahojiano
maalum kuhusu matumizi mabaya ya fedha ambayo yamekuwa yakilalamikiwa
na baadhi ya waumini, vitendo ambavyo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi
wa dini ambao siyo waaminifu na kutumia fedha za misaada kutoka kwa
wahisani kinyume na makubaliano.
Amesema kila kiongozi katika nafasi yake ahakikishe anasimamia haki na
usawa ili kuhakikisha nchi inabadilika kuanzia ngazi za chini hadi ngazi ya
serikali kuu, hivyo pia jamii ya watanzania inapaswa kushiriki katika kusimamia
haki za watanzania wote zinafuatwa na kulindwa bila ubaguzi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia