LEO ni siku ya kuzaliwa kwa ngu mmiliki wa blog ya Libeneke la kaskazini (Woinde Shizza) ni miaka kadhaa hapa duniani imepita sio kwamba mimi ni mwema sana kuliko wale waliotangulia mbele za haki bali ni mapenzi ya mungu ndio yamesababisha leo hii nipo hapa nina afya tele n a nguvu tele
Sifa na Utukufu nazirudisha kwa Mungu maana yeye ndie ajauae sababu ya kuniacha hadi
hii leo kwani sina nilicho mpa mungu wala sina chakumpa zaidi ya kumshukuru kila siku na yote haya naweza sema ni kwa neema tu ndio ilinisababishia nikafika hapa siku ya leo nikaona siku ya leo na nikatimiza miaka ambayo imefika
Napenda kumshukuru sana huyu mungu wangu alieniumba na naomba aendelee kunipigania hadi pale yeye mwenyewe itakavyo mpendeza
Pia napenda kuwashukuru mama zangu wazazi na familia yangu kwa ujumla akiwemo pia mwanangu kwakunifariji ata kwa maneno machache pale anaponiaona nimepungukiwa na kitu sina cha kuwapa zaidi ya kuwaombea kwa mungu aendelee kuwalinda na kuwapigania
"Ndugu zangu mbali na hao niliowataja hapo juu, lakini ninyi marafiki zangu, Wadau wangu, ndugu na jamaa wote popote pale mlipo hapa duniani ni watu muhimu sana sana, hadi kufika hapa leo ninyi mnachango wenu wa namna moja au nyingine sina chakuwa lipa zaidi ya kusema asante na nawaombea kwa mungu aendelee kuwapigania na kuwalinda kila siku na kuwapa afya njema nachoomba tuendelee kupendana kama vile mungu alivyotupenda maana mungu alisema "basi idumu imani tumaini na upendo na katika haya matatu lililo kuu ni Upendo "
Asanteni Mungu awabariki