MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI AGOSTI WAPUNGUA KWA ASILIMIA 4.9

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisi kwake Dar es Salaam leo mchana, kuhusu fahirisi za bei za taifa kwa mwezi Agosti, 2016. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja. 
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo

Na Dotto Mwaibale

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipindi cha mwezi Agosti Umepungua kwa asilimia 4.9 kutoka asilimia 5.1 katika kipindi cha mwezi Julai 2016.

Hiyo inamanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa  kwa mwaka ulioisha mwezi Agosti, 2016 imepunguwa ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwezi Julaai 2016.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa NBS, Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema Nchi zote za Afrika Mashariki kasi ya mfumuko wa bei imepuguwa katika kipindi cha mwezi Agost mwaka huu.

Alisema baadhi ya nchi hizio ni  Kenya Mfumuko wa bei umepunguwa kwa asilimia 6.26 kutoka asilimia 6.36 katika kipindi cha mwezi Julai na Uganda bei imepunguwa kwa asilimia 4.8 kutoka asilimia 5.1 kwa mei Julai Mwaka huu.

"Kupungua kwa mfumuko huo nhini kumesababishwa na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali ya nchi," alisema Kwesigabo .

Alisema mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa z vyakula zilizoonesha kupungua ni pamoja na bei za Samaki kwa asilimia 701, Mafuta ya kupikia kwa asilimia 7.02 na mbogamboga kwa ailimia 6.9.

Pia bidhaa zisizo za vyakula  zilionesha kupunga ni pamoja bei za Gesi kwa asilimia 22.8, Mafuta ya taa kwa asiimia 8.8, dezeli asilimia 9.8 na Petroli asilimia 15.8.

Aidha Fahilisi za bei ambacho hutumika kupima mabadiliko ya bei za huduma mbalimbali  zimepungua kwa asilimia 103.28 kwa mwezi Agosti mwaka huu kutoka 103.50 katika kipindi cha mwez Agosti mwaka 2015.

Alisema kupungua kwa fahilisi za bei umechangiwa hasa na kupungua kwa baadhi ya bidhaa za vyakula ambazo ni nafaka kwa asilimia 0.6, Unga wa muhogo asilimia 2.1, dagaa kwa asilimia 3 na mbogamboga asilimia 2.6.

Hata hivyo alisema thamani ya shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma imefikia sh.96 na senti 83 katika mwezi Agosti mwaka huu kutoka desemba 2015 ilivyokuwa sh.96 na sent 62 kwa mwezi Julai mwaka huu.

Kwesigabo alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi umepunguwa kutoka asilimia 7.6 kwa mwezi Julai hadi kufikia asilimia 7 kwa Agosti mwaka huu.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post