|
Mkurugenzi wa Kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri akizungumza na wakazi wa Kawe kuhusu kampeni ya VIWANDA NI FURSA |
Katika kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya viwanda, Mkurugenzi wa Kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri ameanzisha kampeni mpya ya VIWANDA NI FURSA ambayo itatoa elimu kwa wananchi pamoja na kutoa mikopo ya mashine za viwanda vidogo vidogo kwa wajasiliamali.
Akielezea kampeni hiyo wakati akifanya semina kwa wakazi wa Kawe, Mashauri alisema kuwa ameanzisha kampeni hiyo ili kutoa elimu kwa wananchi lakini pia kuwapa mikopo ya mashine kwani watu wengi wanatamani kufanya biashara lakini wamekuwa wakishindwa kutokana na kukosa mtaji wa kufanya biashara.
Alisema kuwa ili nchi kuwa kufanikiwa kwa kuwa na uchumi mkubwa na kuwa na maendeleo kwa wananchi wake ni lazima iwe na viwanda vingi ili kuwepo ajira za kutosha na shughuli za maendeleo hivyo kupitia kampeni hiyo itaweza kubadili maisha ya watanzania wengi ambao tayari walikuwa wameanza kupoteza matumaini ya kufanikiwa kimaisha.
|
Mkurugenzi wa Kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri akieleza wakazi wa Kawe jinsi wanavyoweza kubadili maisha yao kwa kufanya biashara na jinsi kampuni yake ya HiTECH inaweza kuwapa mkopo. |
"Kampuni ya HiTECH imeanzisha kampeni hiI na itafanyika nchi nzima, serikali tayari imekubali tuifanye kimechobaki ni wananchi wenyewe, tutatoa mikopo ya mashine kwa watakaohitaji na watarudisha kwa riba ndogo ya asilimia 10,
"Ukienda nchi ambazo zimeendelea kama China kuna viwanda vingi, na watu wanajua kiwanda mpaka uwe na eneo kubwa wakati watu hata majumbani wana viwanda na wanazalisha, ni muda sasa watanzania kuchangamkia nafasi hii ambazo HiTECH International imeitoa," alisema Mashauri.
Nae Diwani wa Kawe, Ruta Rwakatare alimpongeza Mashauri kwa uamuzi wa kutoa mikopo kwa wananchi ambao wana malengo ya kufanikiwa kwa kufanya biashara na anaamini kuwa hiyo itakuwa njia moja wapo ya kumaliza vijiwe vya vijana ambao hawafanyi kazi.
"Mimi sipendelei kuona vijana wanakaa tu vijiweni, na sio kwamba wanapenda ila tu sababu hakuna kazi lakini kupitia kampeni ya Paul Mashauri itaweza kuwasaidia kuacha tabia hizo na kuanza kufanya kazi zinazowaletea maendeleo.