kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa
ya fahamu Dr.Othman Kiloloma akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro sehemu ambayo mtoto amefanyiwa upasuaji wa kichwa |
Mkuu wa wilaya ya Arusha akiwasili katika hospitali ya Mount Meru iliopo jijini hapa Tayari kwakwenda kuangalia watoto waliofanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa
kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman Kiloloma akiwa anampa mkuu wa wilaya ya Arusha maelekezo ya picha inayoonyesha jinsi mtoto alivyokuwa kabla ya kufanyiwa upasuaji
mkuu wa wilaya ya Arusha mjini akimkabidhi pampas moja ya mama mzazi wa mtoto ambaye amefanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa ikiwa ni moja ya zawadi walizopatiwa na GSM Foundation
mkuu wa wilaya ya Arusha akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea watoto waliofanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa kikubwa
Na Woinde Shizza, Arusha
Jumla ya watoto 4000 wanazaliwa kila mwaka na tatizo la kichwa kikubwa na
mgongo wazi na kati ya hao ni watoto 500 tu ndio wanafikishwa hospitalini kwa
ajili ya upasuaji huku wengine 3500 awajulikani wanapopelekwa.
Hayo yamebainishwa leo na kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa
ya fahamu Dr.Othman Kiloloma wakati akiongea na waandishi Wa Habari
Mkoani hapa.
Alisema kuwa wao kama taasisi ya moi walikaachini na kuona kunawatoto
wengi ambao wanazaliwa na vichwa vikubwa lakini hawafiki hospitalini kwa ajili
ya garama huku wengine wakiwa wanaamini imani za kishirikina kitu ambacho
sivyo.
Alibainisha kuwa mpaka sasa wameshatembelea mikoa 13 ambayo ni awamu ya
kwanza na wameshafanya upasuaji jumla ya watoto 167 ambapo kwa mkoa Wa Arusha wamewaona
watoto 35 na wamewafanyia upasuaji watoto sita.
"Kila mwaka watoto 4000 wanazaliwa na kati yao 500 tu ndio wanafikishwa
hospitali lakini watoto wanaobaki 35000 atujui wanaenda wapi au wanapelekwa
wapi maana hospitalini awaji"alisema Kiloloma
Kwa upande wao wagonjwa waliofanyiwa upasuaji Wa kichwa Nasson Daniel 17
aliyelazwa katika wodi ya majeruhi wanaume no 3 pamoja na Aisha Amir Suleiman
17aliyelazwa wodi ya majeruhi wanawake wameiomba jamii wasiwafiche watoto wenye
matatizo ndani wawatoe ili wakatibiwe kama walivyotibiwa wao.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi wenye watoto waliofanyiwa upasuaji Emelda
Buxay (36)amesema kuwa amewaomba huduma hii isogezwe karibu na jamii maana
watoto wengi wenye matatizo kama haya wapo vijijini wanateseka na hawana msaada
.
"Wazazi wenzangu haswa wakina mama sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa mud
a mrefu ndiyo tunaweza kugundua mabadiliko ya mtoto ,tusisikilize dhihaka za
watu mtaani ambazo Mara nyingi watu wamekuwa wakisema pale wanapoona mtoto
mwenye ulemavu wowote hebu tuchukue hatua tuwapeleke hospitalini,kama vile
mtoto wangu Dorcus alivyofanyiwa upasuaji leo ni Siku ya tatu kichwa
kinaendelea kupungua ,tusiwafiche watoto jamani "alisisitiza Emelda.
Naye mkuu Wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alitoa wito kwa jamii hususa
ni wazazi kutowaficha watoto wenye tatizo hilo kwani tatizo linatibika na mtoto
anapona kabisa .
Alisema anapenda kuwashukuru madaktari hawa walioibua na kuangalia namna
gani wanaweza kusaidia watoto hawa pamoja na shirika la GSM foundation
ambao ndio waliothamini Huduma hii ya upasuaji bure ambapo alisema kwa
upande wa Arusha jumla ya watoto 35 wameonwa huku watoto sita wakiwa wamekishwa
fanyiwa upasuaji.