Naibu Waziri wa TAMISEMI Sulemani Jafo akihutubia wadau wa kampeni ya kuchangia Madawati Mkoa wa Geita kwenye Harambee iliyofanyika Mjini Geita
Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Elias Kasitila akitoa maelezo kuhusu namna Acacia ilivyoshiriki mwaka huu kuchangia kwenye zoezi la madawati.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Bwana Graham Crew akiwa amenyoosha mikono kusalimia umma wa Watanzania waliongana kwenye harambee ya madawati Geita
Timu ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri baada ya Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Elias Kasitila kutanga kuwa Mgodi utatoa shilingi milioni Mia Moja kwa ajili ya madawati Mkoa wa Geita.
Mgodi
wa Dhahabu Bulyanhulu Umetoa Tsh 100m/- kwa Ajili ya Madawati ya Shule
Mkoani Geita.
Akitangaza
kiwango hicho katika hafla ya changizo iliyofanyika Desire Park Mjini
Geita , Meneja Ufanisi na Mahusiano na Jamii wa Mgodi wa Dhahabu
Bulyanhulu bwana Elias Kasitila amesema, “Bulyanhulu imebarikiwa
kuwa karibu na Wilaya mbili,Halmashauri ya Msalala iliyopo Mkoa wa
Shinyanga na Nyang’wale iliyopo Mkoa wa Geita.
“
Hivyo basi tulipopokea mwaliko kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya
Nyang’wale kuhusu kampeni ya leo ya madawati tumeamua kwamba
japokuwa miradi mingine ya madawati tumeifanya mkoa wa Shinyanga tumeona
kuna umuhimu wa kufanya hivyo mkoa wa Geita pia.”alisema Kasitila.
"Hivyo
basi siku ya leo tunajitolea kuchangia Tsh100m/- kwa ajili ya
kampeni za mikoa inayolenga kuondoa upungufu wa madawati
70,000.”aliongeza Kasitila.
Elias
aliongeza kuwa, “misaada ya madawati kutoka kwenye migodi iliyoko chini
ya Acacia ambayo ni, North Mara, Buzwagi and Bulyanhulu,kwa mwaka huu Acacia
imetumia takriban fedha za kitanzania zaidi ya Billion Moja ambayo
inakadiliwa kutengeneza zaidi ya madawati 10,000.
Mgeni
rasmi katika hafla ya kuchangia madawati mkoa wa Geita alikuwa Waziri Mkuu
wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ambaye aliwakilishwa na Naibu Waziri
Ofisi ya Rais Tamisemi ,Utumishi na Utawala Bora, Mh.Suleiman Jafo.
Akiwahutubia
washika dau waliokuwa Desire park Naibu Waziri Jafo alisema
“Nitapeleka salamu kwa waziri mkuu kuhusiana na mwitikio ambao
nimeushuhudia leo ninaagiza kamati ya Kampeni ya madawati Geita
kuorodhesha washika dau wote waliochangia leo na kuwasilisha orodha hiyo
kwenye ofisi ya Waziri Mkuu ili binafsi awatambue wote walioonesha kuguswa
kuiondolea Geita uhaba wa madawati.”
Katika
hafla hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Aacacia Bulyanhulu Graham Crew binafsi
alijitolea kuchangia fedha za kitanzania shilingi 750,000/- kwa ajili ya
kampeni hiyo.