Mkuu wa wialaya Mh Kasesela akitoa hotuba
Mkuu wa wilaya nakicheza mpira ulio tengenezwa na wajasiliamali wa Ruaha Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Amina Masenza amefungua maonesho ya
wajasiliamali yalio andaliwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard
Kasesela katika barabara ya Olofea Manispaa ya Iringa.
Akifungu
Maonyesho hayo aliwaasa wana vikundi kuwa na umoja ili kufanikisha ndoto
zao.
Pia aliagiza benki ya posta kuhakikisha wanawasaidia mikopo
wajasiliamali hayo.
Mapema akimkaribisha Mkuu wa mkoa , Mkuu wa wilaya
ya Iringa Mh Richard Kasesela alimshukuru Mkuu wa mkoa kwa kukubali kuwa
mgeni rasmi na kumuomba maonesho hayo yawe yanafanyika mara kwa mara
ili wajasiliamali wapate soko na kujikwamua kwa uchumi.
Meneja wa Benki
ya Posta Mkoa wa Iringa Bwana Kayanda aliwambia wajasiliamali pesa ipo
ila wakopaji ndio hakuna hivyo anawakaribisha waje kukopa. zaidi ya
wajasilia mali 600 walipata mafunzo yaliyo andaliwa na Mh Kasesela hapo
tarehe 18/8/16 na leo ilikuwa siku ya kuonyesha bidhaa hizo.
Pia
kilikuwepo kikundi ambacho kinatengeneza mipira ya kuchezea .. mpira wa
miguu cha kata ya Ruaha.