BREAKING NEWS

Friday, September 23, 2016

WAZIRI WA UJENZI PROFESA MBARAWA ATAKA WADAU WA UJENZI WALA RUSHWA WAFUTIWE LESENI ZAO


Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akihutubia wakati akifungua Semina ya 26 ya utoaji elimu endelevu kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dar es Salaam leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Ambwene Mwakyusa akizungumza katika semina hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akipeana mkono na Msaji wa Bodi hiyo Jehad Jehad baada ya kumaliza kutoa hutuba yake.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo.

Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo.

Taswira meza kuu katika semina hiyo.

Picha ya pamoja na mgeni rasmi Waziri Mbarawa.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi, Waziri Mbarawa (aliyekaa katikati), Wengine kutoka kulia waliokaa ni Mkurugenzi wa Huduma na Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Profesa Mhandisi William Nshana, Mwenyekiti wa Bodi, Ambwene Mwakyusa, Msajili wa Bodi, Jehad Jehad na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili, Dk.Adelina Kikwasi.

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa, ameitaka Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuwafutia leseni wadau wa sekta ya ujenzi  watakao bainika kuomba au kupokea rushwa.

Katika hatua nyingine Profesa  Mbarawa ameitaka  Bodi hiyo kuandaa  orodha ya wakadiriaji majenzi na wabunifu  majengo wasiyofuta maadili ya kazi zao ili iwekwe hadharani na wasipate tenda za kufanya kazi popote.

Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati akifungua Semina ya 26 ya utoaji elimu endelevu kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dar es Salaam leo na kueleza kazi yoyote iwe nzuri na bora ni lazima kuepuka rushwa na kufuata  maadili na kanuni za kazi.

“Napenda niwagize bodi kuanzia sasa nataka wakadiriaji majenzi na wabunifu majengo na wadau wote wa sekta ya ujenzi ambao ni wara rushwa muwafutie leseni zao  ili wasiweze kupata tenda au kutoa tenda.Maadili katika kazi zenu ni jambo la msingi na si vinginevyo,”alisema Profesa Mbarawa.

Mbarawa aliigiza bodi hiyo kuandaa orodha ya watakao kuwa  si waadilifu ili kuonyesha katika jamii kuwa hawa hawasitahili kupewa tenda ya aina yoyote. 

Alisema baada ya kuandaa orodha hiyo  ni vizuri ikatangazwe hata katika vyombo vya habari ili iwe fundisho kwa wengine wenye vitendo hivyo.

Mbarawa aliwataka wakadiriaji majenzi na wabunifu majengo nchini kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika serikali ya Awamu ya Tano ili kuweza kjiongezea mitaji.

“Kuna mradi wa ujenzi wa Reli ya kiwango cha kisasa unakuja na serikali imetenga Sh. Trilioni 1, lazima kutakuwa na ujenzi wa majengo hiyo ni fursa mbayo mnaweza kuitumia kujiongezea uwezo, lakini kama mtafanya kazi kwa kuungana njia hiyo inaweza kuwasaidia kupata tenda hizo.” alisema.

Awali, akizungumza katika semina hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ambwene Mwakyusa, alisema semina hizo zimekuwa na faida kwa wakadiriji majenzi na wabunifu, kwani zinawaongezea uwezo wa kujua mambo mbalimbali na kwamba zimekuwa zikifanyika kila mwaka mara mbili na zimewanufaisha wadau wa sekta ya ujenzi 5,328. 



Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates