Spika
wa Bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiingia
katika ukumbi wa Bunge kuongoza kikao cha saba cha bunge la kumi na moja
leo mjini Dodoma.
Spika
wa Bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza
kikao cha saba cha bunge la kumi na moja ambapo pia alisema kiasi cha
shilingi milioni themanini na tano na laki tano zimechangwa kutokana na
makato ya posho ya siku moja yawabunge kwa ajili ya kusaidia waathirika
wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Waziri
wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akimueleza
jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira,
Vijana na watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (MB) picha juu ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe.
January Makamba akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi
na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki wakati wa kikao cha saba cha bunge
la kumi na moja leo mjini Dodoma.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. Selemani Jafo (MB) akijibu swali bungeni ambapo alisema kuwa
serikali itaendelea kupeleka fedha katika serikali za mitaa kwa
kuzingatia hali ya makusanyo ya kila mwezi.
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akijibu
swali bungeni ambapo alitoa wito kwa wabunge kuisaidia kutoa elimu kwa
wananchi waliovamia maeneo ya jeshi kuondoka ili kusaidia kupunguza
migogoro ya ardhi baina ya jeshi na wananchi, wakati wa kikao cha saba
cha bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akijibu swali bungeni
ambapo alisisitiza kuwa Serikali inatekeleza program ya maendeleo ya
Sekta ya maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, wakati
wa kikao cha saba cha Bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Jumanne Maghembe (MB) akimueleza jambo
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina
Mabula (MB), wakati wa kikao cha saba cha Bunge la kumi na moja leo
mjini Dodoma.
Mbunge
wa Jimbo la Mikumi Mhe. Joseph Haule akiuliza swali bungeni kutaka
kujua mikakati ya serikali katika kutatua migogoro baina ya wakulima na
wafugaji inayopelekea mauaji ya raia ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani
Mhe. Mwigulu Nchemba kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi
alisema Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria wale wote
wanaohusika na mauaji ya raia nchini hasa ikiwemo wanaohusika kwenye
migogoro hii.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia