Na Woinde Shizza,Arusha
Nchi za jumuiya wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki chini ya mwenyekiti wa nchi
hizo Dr John Pombe Magufuli hii leo wamepokea hati ya udhibitisho wa nchi ya
Sudani Kusini kuwa miongoni mwa nchi
wanachama wa jumuiya hiyo.
Awali
mapema mwaka huu walitia saini makubaliano ya kutaka kujiunga na kuwa mmoja wan
chi jumuiya wanachama ambapo wataalamu kutoka nchi wanachama ambapo Rais
Magufuli ndiye mwenyekiti kiongozi wa jumuiya hiyo walizingatia vigezo na
masharti vya kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo ambapo leo hii yamekamilika.
Awali
akizungumza mbele ya wajumbe kutoka sudani kusini katibu mkuu wa jumuiya
ya
Afrika Mashariki Liberat Mfumukeko alisema kuwa jumuiya hiyo imepokea
hati ya
uthibitisho wa wanachama wapya wa jumuiya ya Afrika mashariki na kwamba
wanasubiri Mwenyekiti John Magufuli kuidhinisha rasmi katika Mkutano wa
wakuu wa nchi unaotarajiwa kufanyika jijini Daresalaam septemba 8 mwaka
huu.
Kwa upande wake Mshauri wa Rais wa Sudan kusini katika masuala ya Kiuchumi Aggrey
Tisa Sabun ambapo
alisema kuwa wamekuwa wakitamani muda mrefu kuwa nchi wanachama na kwamba
kuleta hati ya maakubaliano ni hatua moja wapo ya muunganiko huo.
Nao Alex mushi na Vailet mushi wanajumuiya ya Afrika mashariki wanasema kuwa Sudani
Kusini Kujuinga na jumuiya hiyo ina faida mbalimbali ikiwemo masuala ya uchumi
lakini pia nchi za jumuiya zinapaswa kufikiri Zaidi na kumaliza machafuko
ambayo yanaendelea katika nchi hiyo kwani hali hiyo inatia ho
Nae Waziri wa
mambo ya nje ushirikiano wa Kimataifa Agustine Maiga ambapo alisema kuwa
wamepokea nyaraka hizo kwa niaba ya Mwenyekiti Rais Magufuli na kwamba
hivi
sasa wanaruhusiwa kushiriki katika vikao vyote kuanzia sasa na wamekuwa
wanachama rasmi wa jumuiya hiyo na watapata fursa mbalimbali kama nchi
mwanachama.
Kutokana
na Sudan ya Kusini kuingia rasmi katika jumuiya hiyo ipo haja ya nchi kuendelea
kuwa wamoja na kwamba waweze kukaa pamoja na kutatua changamoto na machafuko yaliyoko katika nchi hizo , ikiwemo
kutafuta ufumbuzi wa mapigano nchini humo na kuwezesha wanajumuiya kutafuta
fursa za kibiashara nchini humo.