mwenyekiti Wa chama cha wasafirishaji Wa utalii (TATO) wilbroad chambulo akichangia mada wakati wa mkutano
mkutano uliandaliwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wa wadau wa utalii walikutana kujadili changamoto na Tathimini zinazokabili sekta hiyo .
katika mkutano huo pia wakuu wa wilaya zote zilizopo ndani ya mkoa wa Arusha waliuthuria
mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqarro wakifatilia mjadala uliokuwa ukiendelea
Na Woinde Shizza,Arusha
Wadau Wa utalii wameitaka serikali kuweza kuainisha kodi
zote na kuweka katika mfumo mmoja ili kuweza kuepuka usumbufu
unaojitokeza Mara kwamara pindi wageni wanapokuwa katika matembezi yao.
kodi hizo waotozwa katika sehemu mbali hususa ni katika
mageti ambayo wanaingilia watalii mbugani kwani hivi sasa kumekuwepo
na kodi nyingi ambazo zinaleta usumbufu kwa wageni ambapo wanasimamishwa
kila mahali kwa mud a mrefu na kushindwa kufurahia utalii wanaoukuja
kuufanya nchini hapa..
Hayo yameelezwa na mwenyekiti Wa chama cha wasafirishaji Wa
utalii (TATO) wilbroad chambulo wakati akiongea katika kikao cha wadau
wa utalii kilichoandaliwa na mkuu Wa mkoa Wa Arusha cha kujadili
changamoto na Tathimini zinazokabili sekta hiyo .
Aliongeza kuwa mgeni anapofika nchini anatakiwa kupokelewa
kama mfalme sio kusumbuliwa kwa kuwekwa mda mrefu katika viwanja vyetu
vya ndege kwani inawakatisha tamaa na kujutia kuja kutembelea vivutio
vilivyopo hapa nchini.
"Unakuta mgeni anakuja akifika kiwanja cha ndege anakaa
zaidi ya lisaa limoja na nusu kwenye foleni akisubiria visa kweli huu ni
usumbufu ,tunatakiwa mgeni akija hapa tumpokee kwa tabasamu ikiwezekana
tumtandikie zulia jekundu ili akienda kwao atangaze nchi yetu na utalii
wetu kwa ujumla "alisema Chambulo.
Pia aliitaka serekali ifatilie na ishughulike na utozwaji
Wa ada za kodi zinazotozwa na mageti ya wilaya ya Monduli pamoja na geti
la wilaya ya ngorongoro.
"Serekali na Wadau wote tunatakiwa kuweka mikakati
madhubuti kuhakikisha ulinzi na usalama Wa watalii na Mali zao
unaimarishwa zaidi"alisema
Kwa upande wake mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo alisema
kuwa mkutano huo ameuita ilikuwaleta pamoja kushiriki na kujadili namna
gani watakuza utalii na kuboresha utalii katika mkoa Wa Arusha kwa
ujumla na iwapo watashirikiana kwa pamoja itasaidia pia kukuza mapato na
kuwa maradufu zaidi
.
Alisema nivizuri Wadau Wa utalii wakashirikishwa kwa mabadiliko yoyote ya ongezeko la kodi ili baadae kusiwepo na malalamiko ya kuegemea upande mmoja.
.
Alisema nivizuri Wadau Wa utalii wakashirikishwa kwa mabadiliko yoyote ya ongezeko la kodi ili baadae kusiwepo na malalamiko ya kuegemea upande mmoja.
Aliongeza kuwa wao kama mkoa wanamkakati Wa kifunga CCTV
katika maeneo mbalimbali ya mkoa ili kuzibiti uhalifu wanaofanyiwa
watalii au wageni wanaotembelea mkoa wetu pamoja na vivutio vilivyopo
Mkoani apo.
Katika mkutano huo mambo mambali mbali yaliathimiwa ikiwemo
kuitaka serekali na Wadau Wa utalii kuweka mikakati ya ulinzi na
usalama pamoja na kuangalia jinsi ya kuzuia ujangili.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia