Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya vifaa katika chumba cha Maabara ya
hospitali ya Mlele.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akitembelea katika viunga vya hospitali ya Mlele.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akikagua jengo la chumba cha Upasuaji wa hospitali ya
Mlele.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akikagua jengo linalojengwa la chumba cha kuhifadhia
maiti hospitali ya Mlele
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akizungumza na watumishi wa Hositali ya Mpanda.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akikagua stoo ya dawa ya hospitali ya Mpanda.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo katika chumba cha Maabara ya Hospitali
ya Mpanda.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wananchi (Hawapo pichani) wakati wa
ziara yake hiyo katika Hospitali ya Mpanda.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa uongozi wa Hospitali ya Mpanda juu
ya kufanyia marekebisho mapungufu yaliyobainika.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mlele na
kutembelea Hospitali ya Mlele ya Wilaya hiyo pamoja na Hospitali ya
Mpanda iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi huku akitoa maagizo
mbalimbali ya kiutendaji.
Katika
ziara yake katika Hospitali ya Mlele, Dk.Kigwangalla amewaagiza
viongozi wa Serikali wa Wilaya na ule wa Hospitali hiyo kuhakikisha
wanakamilisha mambo muhimu ikiwemo ujenzi wa chumba cha upasuaji, jengo
la kuhifadhia mahiti na vitu vingine huku akitaka ndani ya miezi mitatu
view vimekamilika.
Akiwa
katika Hospitali hiyo ya Mlele, Dk.Kigwangalla ameweza kutembelea sehemu
mbalimbali za hospitali pamoja na kukagua ujenzi wa majengo ya Chumba
cha upasuaji, chumba cha kuhifadhia maiti na majengo mengine ambapo
amemtaka Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanafanya juhudi wanakamilisha kwa
wakati majengo hayo ili wananchi wapate huduma bora.
Kwa
upande wa ziara yake hiyo katika Wilaya ya Tanganyika yaliyopo makao
makuu ya Mkoa wa Katavi, Dk. Kigwangalla ameweza kutembelea Hospitali ya
Mpanda ambayo kwa sasa inahudumia kama Hospitali ya Mkoa ambapo napo
ameagiza kufanyiwa marekebisho mbalimbali ikiwemo kuzingatia masuala
usafi.
Aidha,
ametoa maagizo kuhakikisha wanafunga mfumo wa malipo wa kisasa katika
vyanzo vyote vya mapato ili kukusanya pesa nyingi zaidi zitakazoweza
kuendesha huduma za Afya ndani ya Hospitali hiyo.