Na Woinde Shizza, Arusha
Serikali yaombwa kufungua benki ya viwanda vidogovidogo
itakayowawezesha wajasiriamali na vikundi rasmi kwa lengo la kuviwezeshavikundi
hivyo kupata mikopo yenye riba nafuu
katika shughuli zao za uzalishaji
kwaajili ya maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa taasisis isiyokuwa ya
kiserikali bwana Respicius Timanywa,inayojulikana kwa jina la ,Anti-Porverty and Invironmental Care ,(APEC) inayotoa
mafunzo ya usalama barabarani kwa waendesha
bodaboda nakusisitiza wasitegemee kuendesha bodaboda pekee ila wanayofursa
nyingine ya kuanzisha miradi ya ufyatuaji matofali,ufugaji wa kuku,
mashine za kutotoa vifaranga pamoja na
viwanda vya uzalishaji wa maji na uchimbaji wa visima.
Mkurugenzi wa APEC Nchini Tanzania bwana Respicius Timanywa.
Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo bwana
Moses Mafie katika Wilaya ya Arumeru Kata ya Kikatiti Kijiji cha Sakila
wamebainisha kuwa miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na
kukabwa na kupokonywa pikipiki zao,abiria kukataa kuvaa kofia ngumu,magari
makubwa kuwachomekea wakiwa barabarani sambamba na mwamko mdogo wa baadhi ya
madereva kutokushiriki mafunzo ya usalama barabarani ambao hupelekea kuonekana
kuwa hawana elimu ya usalama barabarani.
Katika hotuba yake mgeni rasmi SSP Nuru Selemani ambaye ni
mkuu wa kikosi usalama cha barabarani mkoa wa Arusha,tafsiri ya serikali
kuruhusuusafiri wa pikipiki maarufu kama
bodaboda ni kurahisisha
usafiri,kuoingeza fursa ajira kwa vijana.
“Lengo kuu la kuruhusiwa kwa usafiri wa pikipiki nchini ni wananchi wetu wasipate taabu ya
usafiri,vijana wetu waweze kujiajiri na kujipatia kipato cha kujikimu kimaisha
na kuepuka kukaa hovyo vijiweni bila kazi” alisisitiza Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa
Arusha.
Aidha amewataka wahitim hao kuwa mfano mzuri wa kutoa elimu
kwa wenzao hata kwenye jamii wanamoishi huku akiwasisitizia kufuata alama zote
za usalama barabarani ili kuepusha ajali .
“Zingatieni alama zote za usalama barabarani,yatumieni
mafunzo yenu kuwalinda na wengine,epukeni ulevi maana ajali nyingi
zinasababishwa na ulevi kwa baadhi ya madereva wa vyombo vya moto,vaeni kofia
ngumupamoja na abiria wenuwapeni kofia ngumu,dereva bora na makini ni yule
anayekifahamu chombo chake,na kuzingatia sheria za usalama
barabarani”alisisitiza SSP Nuru Selemani.
Takwimu za ajali kuanzia januari hadi septemba
mwaka huu zilizoripotiwa ni 445 hivyo amewataka wahitimu kufanyia kazi mafunzo hayo kwa vitendo ili
kuweza kupunguza ajali za barabarani ,mafunzo