Rais Kikwete afungua tawi la KCB Tanzania mjini Moshi

Rais Kikweta akifunua kitambaa kufungua rasmi
tawi la benki ya KCB Tanzania mjini Moshi. Nyuma yake ni Mwenyekiti wa bodi ya Benki hiyo Dr. Edmund Mndolwa
Rais Kikwete akitembelea tawi hilo baada ya kulifungua

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi na wafanyakazi wa tawi hilo la KCB Moshi

Benki ya KCB Tanzania na wateja wake na wananchi wa Moshi mkoani Kilimanjaro Jumatano ilopita walishuhudia kuzinduliwa kwa tawi lao la mjini Moshi na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.

Uzinduzi huo ambao ulikua ni wakipekee kwa Benki hiyo na wateja wake ulifanyika katika ofisi za Benki hiyo iliyopo Baranara ya Boma, Moshi mjini na kushuhudiwa pia na mamia ya wananchi waliokuwa wamesimama kando kando ya barabara.

Tawi hili la Moshi ni miongoni mwa matawi kumi na moja ya Benki hii ambayo ilianzishwa rasmi hapa Tanzania mwanka 1997.

Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Rais aliuagiza uongozi wa juu wa Benki hiyo kupunguza riba za mikopo ili watu wengi waweze kufaidika na mikopo inayotolewa na asasi hiyo na nyingine za kifedha.

Mbali na hayo, Mheshimiwa Rais pia alisema kuwa serikari katika bajeti ya mwaka huu itatoa zaidi ya shilingi bilioni mia moja kwa ajili ya Benki ya uwekezaji ili kuwawezesha watanzania wakope na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande mwengine, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Dk. Edmund Mndolwa alisema kwa upande wake Benki imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja wake na kugusia uanzishwaji wa huduma ya kitechnolojia ya kiBenki ya T24 ambayo itawawezesha wateja wa Benki ya KCB popote katika ukanda wa Afrika mashariki kupata huduma za kiBenki popote ilipo Benki hiyo ya KCB.

Naye mkurugenzi mkuu wa Benki hiyo nchini Nd. Joram Kiarie mbali na kuwashukuru wateja wa Benki hiyo kwa kufanya biashara nao, pia aliwasihi wale wote ambao bado hawajapata fursa ya kuhudumiwa na Benki hii, wafanye hivyo ili waweze kufaidi na kufurahia huduma bora zinazotolewa na Benki hiyo.

Benki ya KCB ndio Benki kubwa kwa rasilimali katika ukanda wa Afrika Mashariki na ni Benki kubwa ikiwa na matawi zaidi ya mia mbili (200) na mashine za kutolea pesa yaani ATM zaidi ya mia nne (400).


About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia