TAASISI ZA UTAFITI WA MBEGU ZAHIMIZWA KUWAFIKIA WAKULIMA

TAASISI za Utafiti wa mbegu nchini zimetakiwa kuhakikisha kuwa teknolojia ya utafiti wa mbegu bora za mazao mbalimbali zinawafikia wakulima ili waweze kuzalisha mazao na kupata tija katika kilimo.

Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa Utafiti wa maendeleo ya mbegu za kilimo kanda ya kaskazini, Dr Lucas Mugendi, alipokuwa akifungua warsha ya siku mbili kwa wataalamu wa kilimo kutoka Tasisi za utafiti wa Sekretariet za mikoa , halimashauri za wilaya na sekta binafsi .

Dr Mgendi,amesema kuwa katika taasisi hizo za utafiti kuna hazina kubwa ya teknolojia mbalimbali za kuboresha kilimo na ufugaji, lakini tatizo ni kuwa, teknolojia hiyo zimekuwa haziwafikii wakulima kwa wakati na hivyo kushindwa kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo nchini.


Akitolea mfano amesema ni asilimia10 tu ya mbegu ndio zilizofanyiwa utafiti na kuwafikia wakulima ,wakati asilimia 90 mbegu za asili ambazo hazijafanyiwa utafiti wakulima wanazitumia kuzalishia mazao mbalimbali na hivyo hawawezi kupata tija kubwa katika kilimo chao.

Dkt, Mugendi, amesema nchi yetu inakabiliwa na changa moto mbalimbali za hapa na pale zikiwemo za usambazaji na matumizi ya kiwango kidogo cha teknolojiaza kisasa ,zilizozalishwa na vituo vya utafiti vya Tacri, TPRI, Camartec, Sari,na Hort Tengeru ,

Amesema kuwa kutokana na changamoto hiyo ya kufikisha teknolojia kwa wakulima wataalamu hawana budi kuwafikia wakilima ili kuweza kuwasaidia kuzalisha mbegu bora kwa kutumia teknolojia ili waweze kuongeza uzalishaji

Ameziomba halimashauri za wilaya pamoja na sekta binafsi kuweka bajeti kwa ajili ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa maazimio kila mwaka ili kuwezesha wakulima wafugaji na wagani vijijini kufaidika nazo.

Awali mratibu wa warsha hiyo, Jeremih Sembose, amesema kuwa Warsha hiyo ni mwendelezo wa Warsha iliyofanyika Feburuari 4 na 5 mwaka 2010 iliyohusu usambazaji wa tafiti zilizozalishwa na kusambazwa kutoka ngazi ya kanda hadi halimashauri .

Amesema kuwa bado upatikanaji wa mbegu bora ni tatizo kubwa kwa wakulima vijijini ,pia ushirikiano wa wadau wa kilimo na mifugo hauridhishi ,kwa sababu hakuna uwazi wala ,taratibu nzuri za ubadilishanaji taarifa kwa sababu kuna urasimu licha ya kuwepo hazina ya takwimu nyingi

Sembose,amesema kuwa malengo ya jumla kuhusu Warsha za kilimo kwa kanda ya kaskazini ni kuziwezesha wilaya na wadau wa kilimo kuelewa na kuzitumnia teknolojia zilizopo katika vituo vya utafiti katika mpango wa kuboresha kilimo na ufugaji nchini.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia