WAFANYABIASHARA WALIA NA RIBA KUBWA KWENYE MABENKI



Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kibishara wajasiriamali wa klabu ya wafanyabiashara ya benki ya NMB mkoa wa kilimanjaro,(NMB business Club)aliyesimama ni meneja wa NMB kanda ya kaskazini,Vicky Bishubo akijibu baadhi ya maswali yalioulizwa na washiriki hao jana mjini moshi.

WAFANYABIASHARA wadogo, wameziomba taasisi za fedha hususani mabenki yanayotoa huduma ya mikopo nchini,kuangalia uwezekano wa kupunguza riba ili kuwawezesha kumudu uendeshaji wa biashara zoa na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.

Wafanyabiashara hao wadogo na wakati wametoa rai hiyo,baada ya kuhudhulia mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kibiashara ,yaliyokuwa yakiendeshwa na benki ya NMB mjini Moshi, kwa wafanyabiashara ambao ni wanachama wa klabu ya benki hiyo(NMB Business Club) wa mkoa wa kilimanjaro.

Mwenyekiti wa Klabu hiyo,Valerian Kyayu alisema kuwa taasisi hizo za fedha iwapo zitaona umuhimu wa kuwapunguzia riba baada ya kuwapatia mitaji ,zitawasaidia sana kuendesha biashara zenye tija.

Alisema hatua hiyo itasaidia kumudu marejesho ya mikopo yao,tofauti na sasa ambapo wafanyabishara wengi wamekuwa wakikwama kutokana na kutozwa riba kubwa.

Ingawa aliipongeza benki ya NMB kwa kuendesha mafunzo ya mara kwa mara ya kuwajengea uwezo wa kibiashara ,aliitaka pia benki hiyo kuangalia uwezekano ya wanachama wake kuwapa upendeleo wa kuwapunguzia riba ya mikopo wanayoichukua hatua ambayo itawasidia kuweza kujiendesha hapo baadae bila kutegemea mikopo.

Hata hivyo alisema kuwa wafanyabaishara wadogo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi na kujikuta wakishindwa kumudu kurejesha mikopo,ambapo ni pamoja na uelewa mdogo wa kufanyabiashara kitaalamua ,mchanganuo wa biashara na elimu juu ya biashara na masoko.

Aidha ameitaka benki hiyo kuendelea kutoa mafunzo hayo kwa wafanyabishara hao,ili waweze kumudu kuendesha biashara yenye tija ,na wameitaka benki hiyo kutosita kuwapatia mitaji ya kutosha kwa kuwa wengi wao wamekuwa na uelewa mkubwa wa biashara baada ya kupata mafunzo hayo ya mara kwa mara.

Kwa upande wa meneja wa NMB kanda ya kaskazini,Vicky Bishubo aliwahakikishia kuwa, benki hiyo itahakikisha inatekeleza yale yote yaliyo nje ya uwezo wake ikiwemo kuongeza kutoa mikopo mikubwa zaidi kwa wanachama wake.

Hata hivyo alisema suala la kupunguza riba atahakikisha analifikisha kunakotakiwa ili linafanyiwa kazi na wateja wake waweze kunufaika zaidi na mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na benki hiyo.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia