TBL YATOA 1.5 MILIONI KWA TIMU YA MKOA WA ARUSHA



Picha kaimu katibu tawala wa mkoa aliyevaa suti nyeusi akimkabithi mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha (ARFA)Halfa mgonjwa fedha ambazo wamepewa na TBL kwaajili ya maandalizi ya tim




kaimu katibu tawala wa mkoa wa Arusha Twariel Mchome alievaa suti nyeusi akipokea msaada wa fedha zilizotelewa na kampuni ya TBl shilingi 1.5 kutoka kwa meneja matukio wa tbl kanda ya kaskazini mashariki George mwombeki kwa ajlili ya maandalizi ya timu ya mount meru woriiusi ambayo inashiriki mashindano ya kili taifa cup


Timu ya Mounti Meru woriasi ya jijini hapa imepatiwa imepatiwa shilingi milioni moja na nusu kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya kili taifa cup ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni



Akikabidhi msaada huo wa fedha hizo meneja matukio wa TBL kanda ya kaskazini mashariki George Mwombeki alisema kuwa kampuni yao kwakupitia kinywaji chao cha Kilimanjaro wamekuwa na kawaida ya kuzamini mashindano haya kila mwaka.

Alisema kuwa fedha hizo ambazo wamezitoa ni kwaajili ya timu hiyo kujiandaa na mashindano ya Kilimanjaro taifa cup ambayo yanashirikisha mikoa 24 ya hapa nchini na katika mikoa hiyo kila timu ya kila mkoa itapewa fedha hizo na kampuni hiyo.

Akipokea msaada huo kaimu katibu tawala wa mkoa wa arusha Twariel Mchome alisema kuwa anawapongeza kampuni hii ya bia ya TBL kwa kuandaa mashindano haya na kuwathamini kwani mashindano haya yanawapatia vijana ajira.



Alisema kuwa kuendesha michezo ni garama hivyo kampuni kama hii iliyojitolea kuthamini haya mashindano inasitalii kupongezwa huku akiwasihii watu mbalimbali kuendelea kujitokeza kuthamini michezo ili kuweza kuwapatia vijana ajira.



‘’unajua michezo kama hii ni ajira hivyo watu mbalimbali wajitokeze kuthamini mashindano kama haya kwani vijana wetu wakienda kushiriki ata idadi ya vibaka itapungua kwani ule mda ambao wanaenda kupanga kuiba watautumia kwenda kucheza michezo hii”alisema mchome.



Kwa upande mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha(ARFA) Halfa mgonja alisema kuwa anawashukuru Tbl kwa kuwapa msaada huu na timu mpaka sasa ipo kambini kwa ajili ya kujiandaa na mashindan o haya ambayo yanaanza hivi karibuni.



Alisema kuwa timu yao ya mkoa ya Mounti meru imepangiwa katika kituo cha Kilimanjaro ambapo alibainisha kuwa kwakuwa wao ni wenyeji wa mashindano haya kuanzia hatua ya robo fainali hivyo wameandaa vijana wazuri ambao wataacheza vyema na kombe kubaki hapa mkoani.



“kwakuwa sisi ni wenyeji wa kuanzia robo fainali tumandaa vijana ambao watacheza vyema na kufanya kombe la kili taifa cup kubaki mkoani hapa “alisema mgonja.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia