JESHI la polisi mkoani Manyara limepunguza kwa kiwango cha
makosa ya uhalifu toka 2,278 hadi kufikia 2143 kati ya matukio ya uhalifu
yaliyotokea katika kipindi cha kutoka Januari hadi kufikia Desemba 2011
na yale ya mwaka 2010.
Hayo yameelezwa na mwakilishi wa kamanda wa polisi mkoani
humo Moris Okinda wakati akitoa mada ya
hali ya uhalifu na dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi mkoani manyara
kwenye mkutano wa wadau wa habari na waandishi uliofanyika juzi-januari 20
mjini babati uliofunguliwa na mkuu wa mkoa huo Elaston John Mbwillo
Akitoa taarifa hiyo Okinda alitaja matukio hayo yametokana na
vitendo vilivyokithiri vya ubakaji,wananchi wenyeji wa mkoa huo kutembea na
silaha,ubakaji,unywaji na uuzaji wa pombe haramu ya moshi,utupaji wa
watoto,wizi wa mifugo na matumizi ya dawa za kulevya kama vile bangi na
mirungi.
“uchambuzi umefanyika na kubaini kwamba matukio mengi
yanakwenda sambamba na unywaji wa pombe haramu ya moshi na baadhi ya makosa
hutokana na vitendo vya mila na desturi za kutembea na silaha za jadi katika
mikusanyiko ya watu wengi kama vile vilabu vya pombe,magulio na minada”Alisema
Okinda
Katika ufafanuzi wa taarifa yake Okinda alisema matokeo hayo
ya ukusanyaji wa taarifa yanaonyesha kuwa maeneo yaliyofanyiwa kazi na kufanikisha
kupungua kwa makosa 135 tofauto na mwaka 2010 yametokana na kuwepo kwa juhudi
za wadau mbalimbali kwa kutumia dhana ya polisi jamii na Ulinzi shirikishi.
“mwaka huu tumepunguza matukio ya uhalifu toka mwaka
2010 hadi kufikia 2011 kwa kipindi hicho tumepunguza makosa 135,lakini hii
imetokana na matumizi ya fursa zilizotumika kupitia mpango wa ulinzi
shirikishi”Okinda
Aliongeza kuwa matukio hayo ya uhalifu yanongeza unyanysaji
wa kijinsia hasa kwa wanaume walio wengi kuwanyanyasa mabinti wa kambo kwa kuwabaka
kwa nguvu inayotokana na vitisho vya mauaji jambo ambalo pia linaelezwa kuwa
huenda likasababisha ongezeko la magonjwa ya zinaa kwa wanaonyanyaswa.
“unywaji wa pombe haramu ya gongo umechangia vitendo vya
ubakaji…hasa ukiangalia wale waliooa wanawake waliokutwa na watoto wa kike
hawaoni haya kutembea na watoto wa kambo jambo ambalo ni bay asana katika jamii
zetu za kiafrika na unyanyasaji kwa mtoto wa kike”.Alibainisha Okinda
Aidha Okinda alisema matukio ya uhalifu huenda yasimalizike
endapo hakutakuwa na fursa zitakazoweza kutumiwa kuuzuia ikiwa kama katiba mpya
itakayoundwa haitaweka Ibara itakayosimamia sheria za serikali za mitaa na sera
za taifa zinawezesha kuwepo kwakusimamia fursa hizo bado matukio hayo
yataongezeka..
Amezitaja baadhi ya fursa hizo kuwa ni kuwepo kwa mfumo wa
kamati ya ulinzi na usalama katiak ngazi za kata,vijiji na mitaa ikiwa ni
pamoja na askari wa jadi na mgambo na sheria inayotambua na kuanzisha mkakati
wa kuzuia na kupunguza uhalifu mijini utakaohusish halmashauri ambazo ziandaa
bajeti.
Awali akifungua mkutano huo mkuu wa mkoa huo Elaston John
Mbwillo amezitaka taasisi na asasi mbalimbali kutumia vyombo vya habari
kuielimisha jamii kuhusu athari za uhalifu pamoja kwasababu ndivyo vyenye nguvu
kubwa ya kuwafikia wananchi wote na kuacha ubinafsi.
“haya tumealikwa kusikiliza kile tulichoitiwa hapa..ni kweli
vyombo vya habari ni mhimili wan ne wa dola lakini baadhi ya watendaji wa
serikali wamekuwa wakikwepa vyombo vya habari kwangu mimi siafikiani nalo
vitumieni vyombo hivyo ili viweze kuelimisha jamii nzima”
Hata hivyo katika mkutano huo uliojumuisha wadau 70 ulileta
faraja kwa klabu hiyo iliyojipatia zaidi ya shilingi milioni 12 zilizopatikana
kwa njia ya harambee baada ya wadau hao kukiri kuwepo kwa mazingira magumu ya
utendaji kazi hasa ikizingatiwa kukosekana kwa utaratibu wa wamiliki wa vyomb
hivyo kutowathamini kwa kuwapa vitendea kazi huku wakitegemea kuendesha
biashara zao.
Katika hotuba iliyotolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo ya
MAMEC Ben Mwaipaja ameeleza changamoto zinazoikabili klabu hiyo kuwa ni wengi
wao kutokuwa na vitendea kazi badala ya wamiliki kuwatelekeza kwa kutotambua
umuhimu wao huku wakiendesha biashara zao kwa kutegemea vitendea kazi
vinavyotokana na jitihada binafsi za mwandishi mwenyewe.