BREAKING NEWS

Wednesday, January 25, 2012

MMBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI AZIKWA


Spika wa bunge la Tanzania Anna Makinda akiwa nafarijiana na mbunge wa upinzani Zitto kabwe katika mazishi ya mbunge wa Arumeru mashariki
Spika Anna makinda akiteta jambo na spika mstaafu Samweli sita katika msiba wa  mbunge Sumari
Waziri mkuu akiwasasalimu baadhi ya wabunge waliokuwa katika msiba huo mara baada ya kuwasili katika msiba huo
huu ni msiba wetu sote kwakeli tunatakiwa tumuombee hapo muheshimiwa lowasa wakiteta
familia ya marehemu Jeremiah Sumari ikiwa ikiwa imeketi katika mazishi hayo msatari wa mbele kabisa ni mke wa marehemu sumari wa pili kutoka kushoto akiwa na watoto wake
Waziri wa jamuhuri ya muungano Tanzania Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu
Spika wa bunge akimfariji mke wa marehemu sumari katika msiba huo
Mwenyekiti wa IPP Media Reginal Mengi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu
waombolezaji wakiwemo wabunge walikuwemo pia katika msiba huo
Muwakilishi  wa upinzani Zitto kabwe akitoa salamu za rambirambi kutoka katika chama cha Chadema
Mke wa marehemu akiwa na watoto wakijifariji mara baada ya kuaga mwili wa baba yao
watoto wa marehemu pamoja na mke wakiimba wimbo wa kumuaga baba yao
Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Jakaya mrisho Kikwete wakiwa wameongozana na spika wakielekea makaburini
Mke wa marehemu katika kati akiwa amekaa kwa uzuni wakati mwili wa marehemu mume wake ukiwa unawekwa kaburini
vijana wa chama cha mapinduzi wakiwa wanafukia kaburi la mbunge sumari
  
Spika wa bunge Anna Makinda akiweka shada la maua


Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la mbunge Sumari


MAZISHI ya  aliyekuwa  Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Jeremiah Sumari amezikwa jana kijijini kwake Akeri wilayani Meru Mkoani hapa na mazishi hayo kuongozwa na Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya kikwete, pamoja na waziri mkuu Bw Mizengo Pinda, huku mazishi hayo yakiingiliwa na doasari ya mtizamo tofauti wa chama cha mapinduzi(CCM) na chama cha Demikrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Dosari hiyo ilitokea mara baada ya mazishi kumalizka ambapo mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Bw Goodbless Lema alipopita na kuonesha ishara ya chama hicho ambapo hali hiyo ilizua mtafaruku kwan wananchi wa jimbo hilo ambalo lipo chini ya CCM.

Aidha  baada ya wananchi ambao walikuwa katika eneo hilo la mazishi walianza kuonesha ishara  mbalimbali za kumpinga mbunge huyo na baadhi ya wafuasi wake hali ambayo ilisababisha vurugu kubwa .

"leo tunamzika mbunge wetu ambaye ametusaidia na bado hatujasahau ni dakika 30 baada ya kuzikwa halafu ishara ya upinzani inakuja sasa hatupo tayari kwa chama kingine kabisa sisi ndio wameru hatutaki kampeni kwenye misiba kabisa "walisema wananchi  hao.

Pia baada ya kuonekana kwa vurugu hizo ambazo zilidumu kwa muda wa dakika 25 Mbunge huyo aliondoka katika eneo hilo la Msiba  hali ambayo ilifanya taratibu zingine ziweze kuendelea chini kya viongozi wa serikali.

Naye  Waziri mkuu akiongea  na waombolezaji waliofika katika eneo hilo la Akeri  alisema kuwa viongozi mbalimbali wa Serikali wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kama alivyokuwa  Bw Sumari kwa kuwa alijitolea kusaidia serikali katika mambo na mipango mbalimbali.

Bw Pinda alieleza kuwa kiongozi kama kiongozi anatakiwa kuwa na sifa ambazo zitamfanya jamii imkumbuke mara zote na sifa hizo zinatakiwa kuwa ni miongoni mwa sifa nzuri na zenye kulijenga taifa.

“hii ni safari ya mwisho ya   Bw Sumari lakini sote tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunaweka hazina hapa duniani, na kuwa na sifa nzuri na zenye kupendeza, kwa kuwa kifo ni msingi wa kila mwanadamu hapa duniani”aliongeza bw Pinda.

Pia aliitaka familia ya Marehemu Sumari kuhakikisha kuwa haioni mzigo kwa kuondokewa na Baba yao na badala yake wahakikishe kuwa wanaendelea kumtegemea zaidi Mungu katika mambo yao ikiwa ni pamoja na kufuata Mambo mazuri ambayo yalikuwa yanafutwa na Bw Sumari.

Katika hatua nyingine viongozi mbalimbali ambao waliongoza ibada hiyo ya Mazishi walisema kuwa kwa sasa jimbo la Arumeru Mashariki limepoteza Mbunge wake kwa maana hiyo ni lazima taratibu za kumtafuta Mbunge huyo zifanyike wakati utakapofika lakini wagombe wanatakiwa kuwa makini na kuachana na tabia ya uchakachuaji wa matokeo.

Walibanisha kuwa endapo kama zoedzi la uchakachuaji wa matokeo katika jimbo hilo ni wazi kuwa watakuwa wanaweka jimbo hilo mashakani kabisa hali ambayo itachangia matatizo mbalimbali juu ya jimbo hilo.

“tunatangaza rasmi kabisa kuwa hapa hamna masuala ya kuchakachua matokeo kwa maana hiyo uchaguzi utakaokuja ni lazima matokeo yawe ya halali kwa maslahi ya jimbo hili”waliongeza wachungaji hao.

Aidha nao  viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) walisema kuwa wao kama chama kupitia kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo walikuwa na ahadi nyingi dhidi ya jimbo hilo ambapo ahadi hizo zilikuwa na lengo la kusaidia jamii.

Walisema kuwa ahadi za mbunge huyo kwa jimbo hilo ziko palepale na zitatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya chama hicho kwa eneo  hilo la Arumeru Mashariki ili kuweza kupambana na changamoto mbalimbali



Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates