WAFANYAKAZI WA TPC WAOMBA WAOMBA SEREKALI IWASAIDIE MAFAO YAO

WAFANYAKAZI wa kiwanda cha sukari cha TPC cha wilayani Moshi wameiomba
wizara ya kazi na ajira kuwasaidia wastaafu waliokuwa wanachama wa
mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF wa kiwanda hicho wanalipwa mafao yao.

Ombi hilo lilitolewa hivi karibuni kwa naibu waziri wa kazi na ajira
Dk Makongoro Mahanga wakati alipotembelea kiwanda hicho kijionea
shughuli za uzalishaji wa sukari ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku
10 kutembelea maeneo mbalimbali ya kazi katika mikoa ya Tanga Arusha
na Kilimanjaro.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa kiwanda hicho,mwenyekiti wa
chama cha wafanyakazi huduma za jamii Tanzania tawi la TPC  Bilal Juma
alisema  huduma zinazotolewa na baadhi ya mifuko ya kijaamii
haiwatendei haki wastaafu .

“Mh Naibu waziri nipende kufikisha kilio hiki cha wafanyakzi wa TPC
ambacho sasa kimekuwa ni kero kubwa pindi wanapostaafu,hii ni kuhusu
baadhi ya mifuko ya hifadhi ya jamii hususani NSSF ambao kwetu sisi
umekuwa ni kero ya muda mrefu”alisema Juma.

Alisema mfuko huo umekuwa ukichukua michango ya wafanyakazi kila mwezi
pindi wafanyakazi wanapofikia umri wa kustaafu na kuanza kufuatilia
mafao yao hupewa fomu ya maombi ya kujitoa uanachama.

“Leo hii ukistaafu katika ajira yako ukienda NSSF ukitaka mafao yako
unatakiwa kujaza fomu iliyoandikwa fomu ya kujitoa uanachama hali
ambayo inatutaiza na hatui hasa lengo la mifuko hii ya kijamii”alisema
Juma.

Juma alisema zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wa TPC ni wanachama
katika mfuko wa kijamii wa NSSF lakini hakuna mstaafu aliyestaafu TPC
na kupewa mafao yake na NSSF jambo ambalo linawakatisha tamaa ya kuwa
wanachama.

Kwa upande wake naibu waziri wa kazi na ajira Dk Mahanga akitolea
ufafanuzi suala hilo kwanza aliipongeza NSSF kwa kuwa na mafao mengi
tofauti na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.

“Kabla ya kulaani ,kwanza niwapongeze NSSF kwa kuwa na mafao saba sasa
yanayotolewa kwa jamii,lakini pia unaweza kuwa na mafao mengi kati ya
hayo sita yanaweza kuwa mazuri moja likawa si zuri”.alisema Dk
mahanga.

Dk Mahanga alisema kuwa kilio hicho amekipokea na kuwa atakifikisha
katika mamlaka husika ili kuweza kutoa suluhu kwa wafanyakazi
kiwandani hapo.

“Inawezekana malalamiko haya si hapa TPC peke yake ,niwahahakishie
ndugu zangu hili nalichukua maana na hakika halipo kwenye mikataba ya
NSSF talipeleka ngazi ya juu tuone ni namna gani tunaweza
kulishughulikia.”alisema Dk Mahanga.

Alisema hivi sasa kimeundwa chombo kitakachodhibiti  mifuko ya jamii
nchini kitakachoandaa taratibu za kuishauri mifuko hiyo ili mafao yake
yasiwe na tofauti na yatozwe kwa aina moja .

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post