FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO LA HAI ZAGUBIKWA NA UTATA MTUPU

MJUMBE  wa kamati ya mahesabu ya Serikali  (LAAC), Subira Mgallu
amesema kuwa hatakikisha kuwa anafuatia matumizi ya fedha za mfuko wa
jimbo katika jimbo la  Hai mkoani Kilimanjaro kutokana fedha hizo
kugupikwa na utata juu ya matumizi yake

Kauli hiyo inakuja baada ya kudai kuwa tangu serikali ya awamu ya  nne

kuingia madarakani fedha za mfuko wa jimbo zinazotolewa na serikali
katika jimbo hilo hazijawahiu kutolewa kwa ajili ya matumizi
yaliyokusudiwa kutokana na Mbunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe
(CHADEMA) kuzimiliki

Mgallu ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu (CCM), mkoani Pwani,

alisema fedha za mfuko wa jimbo  zinatakiwa kutumika kwa wakati
uliokusudiwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na si kumilikiwa na
mbunge kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki za wananchi na kuendelea
kudumaza maendeleo

Akizungumza na wananchi wa kata za Masama Mashariki na Masama

Magharibi katika ziara yake kuhamasisha wananchi juu ya uundwaji wa
katiba mpya,na kutoa ufafanua juu ya upotoshaji Unaonezwa  baadhi ya
wanansiasa yanayolenga kuvunja utaratibu uliowekwa na Serikali iliyopo
madarakani

Alisema, Mbowe kushindwa kutoa fedha hizo kwa kipindi chote tangu

alipochaguliwa katika nafasi ya Ubunge Oktoba 31 mwaka 2010 ni kinyume
na utaratibu kwani fedha hizo zinatolewa kwa makusudi maalumu ya
kupunguzia wananchi matatizo yaliyopo katika kata,vijiji kwa ajili ya
kuboresha huduma za kijamii

Alisema  katika jimbo la Hai jumla ya shilingi milioni 18 zinatolewa

lakini  fedha hizo zinashindwa  kuwafikia walengwa wakati katika
majimbo mengine wananchi wamekwisha faidika na fedha hizo ambapo
waweza kuboresha huduma zao  na kupatikana kwa uhakika kwa kupitia
fedha za mfuko huo



“Fedha zinazotolewa na serikali, utaratibu wa matumizi upo wazi lakini

zitumie kwa malengo yalikusudiwa kwa kufuata sheria na kusimamiwa na
kamati maalumu ya wajumbe  7 akiwemo Mbunge Mwenyewe ….nashangaaa
kusikia mpaka sasa fedha hizo hazijatumika na wala hakuna wajumbe wa
kamati hiyo katika jimbo hilo ”alisema Mgallu

“Ndugu wananchi jambo hilo lazima tulifikishe katika kamati yetu

iliyochini ya Mbunge wa Vunjo, Augostino Mrema ili tujue fedha za
mfuko wa jimbo zimeenda wapi? Na endapo zipo kwa nini hazijatumika
mpaka sasa na zinasubiri nini kutumika ?”alihoji Mbunge huyo

Alieleza kuwa Serikali inatambua matatizo ya wananchi, ndio maana

ukawepo mpango wa kutoa fedha kwa jimbo kupitia mbunge aliyepewa
ridhaa ya kuliongoza, lakini Mbowe amekuwa akizikalia kama za kwake,
hali inayorudisha nyuma maendeleo.

“Kuna matatizo mengi vijijini na fedha za wananchi tayari

zimeshatolewa na Serikali, sasa natoa mwezi mmoja kwa Mbowe
kuhakikisha amezigawanya fedha hizo kwa kila kata kwa lengo la
kusaidia wananchi hususani vijana,” alisema Mgallu.

Kunakana na ufafanuzi uliotolewa na Mbunge, wananchi wa kata hizo

walisikitishwa na kitendo hicho ambapo Mchungaji wa KKKT, Barnabas
Munuo aliiomba serikali kuliingilia kati suala hilo kwa wananch
wamekuwa hawatendewi haki na wawakilishi wao na kukumbatia fedha za
wananchi pasipo sababu maalumu

Munuo alisema shule nyingi zinakabiliwa na matatizo ya vyumba vya

madarasa wakati serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuwasaidia wananchi
kuepukana na michango ya mara kwa mara jambo ambalo kinyume na
taratibu na makusudio ya fedha hizo na kuwataka kamati husika kufanya
uchunguzi wa kina juu ya suala hilo.

Naye Mwenyekiti   wa kamati ya  LAAC  Taifa, Mrema alisema kutofikisha

fedha hizo kwa wananchi ni kosa kubwa kwani fedha hizo, zimetolewa kwa
ajili kuchangia shughuli za kimaendeleo na si mtu binafsi kumiliki
fedha hizo.

Mrema alisema kutokana na taarifa hizo atahakikisha kamati yake

inafanya ukaguzi wa haraka ili kubaini kuwa fedha hizo zipo wapi na
endapo zitajulikana kutumika kinyume na utaratibu mhusika atafikishwa
katika vyombo vya dola

Hata hivyo juhudi za kumpata,Mbunge wa jimbo  la Hai, Freeman Mbowe

kuelezea tuhuma hizo ziligonga mwamba  baada ya simu ya kiganjani
kuita bila ya kupokelewa

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post