No title



KWA WANACHAMA WOTE WA APC.

Husika na kichwa cha habari hapo juu. Ukiwa mwanachama wa APC
unajulishwa kwamba Januari 28, Mwaka huu kutafanyika Mkutano Mkuu wa
dharura.

AGENDA za mkutano huo zitakuwa ni,
1- Mabadiliko ya Katiba ya APC
2- Ripoti ya fedha ya Mwaka 2010.

Kutokana na umuhimu wa Mkutano kwa Klab, ndugu mwanachama unakumbushwa
kulipia ada yako ya mwezi unayodaiwa ili uweze kuwa mwanachama hai na
mwenye sifa za kuhudhuria mkutano huo. Bila kulipia ada yako hautakuwa
na sifa za kuhudhuria mkutano, hii ni pamoja na kwa viongozi.

Tafadhali lipa ada yako sasa.

Taratibu za kufanyika kwa mkutano huu zinaendelea kufanywa.
Nitawajulisha hapo baadae eneo husika la mkutano na muda wa kuanza
mkutano.

Kwa pamoja tushirikiane kuijenga APC na si kuivunja.

Natanguliza shukrani zangu kwako.

Asante.


Eliya Mbonea
KATIBU MKUU -APC

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post