WAPANGAJI wa jengo
linalomilikiwa na kanisa la kiinjili,kilutheri Tanzania(KKKT)dayosisi
ya mjini kati jijini Arusha,wanatarajia kumfikisha mahakamani mpangaji
mwenzao ambaye ni benki ya CRDB tawi la Meru na meneja wa jumba hilo
kutokana na kukiukwa kwa mkataba wa upangaji unaofanywa na benki hiyo
kwa kushirikiana na meneja wa jengo.
Wakizungumza kwa jazba jana ,wapangaji hao wamedai ya kuwa benki ya CRDB imekosa ustaarabu wa kibiashara,kwani imekuwa ikiwanyanyasa kwa muda mrefu wapangaji wengine kwa kuweka vibao vya benki hiyo kila mahala katika milango ya ofisi za wapangaji hao bila kujali kwamba wao wanahaki kama benki hiyo kupanga katika jengo hilo lililiopo karibu na hotel ya New safari mjini kati,na kuwafanya wakose wateja ambao wamekuwa na woga wa kuingia kwa kujua ni benki.
Walisema tangu benki hiyo ipengishwe katika jengo hilo imekuwa ikiwanyanyasa ikiwepo kuziba milango yote ya kuingilia kwa matumizi ya benki na wao kubaki na mlango mdogo mmoja ,kiasi kwamba iwapo kutatokea hitilafu ya umeme ama kuungua kwa jengo hawatakuwa na uhuru wa kutoka.
Mmoja wa wapangaji hao,Richard Paulo ambaye anaofisi ya kukusanya madeni ya Marcas Investiment,alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikipewa kiburi na meneje wa majengo hayo,Darius Bipa ,kwani pamoja na malalamiko yao ya muda mrefu kuyafikisha kwa meneja huyo na uongozi wa benki,wamekuwa wakipuuzwa na kuonekana kama hawana haki ya kupangisha katika jengo hilo.
''huu sio ustaarabu hata kidogo ,lazima tuifikishe mahakamani benki hiyo na tayari tumewasiliana na mwanasheria wetu kwa hatua zaidi,tumelalamika muda mrefu hawatuelewi wala kutusikiliza hivi sasa hatupati wateja, watu wanaogopa kuingia ndani ya jengo ,wanajua hiyo ni sehemu ya benki''alisema Paul
Mpangaji mwingine,aliyejitambulisha kwa jina la mama Kanana,ambaye anamiliki duka la nguo na vipodozi,alisema kuwa kuwekwa kwa vibao vya benki kwenye milango ya ofisi zao kunawakosesha wateja ,kwani kila mtu atakayefika katika jengo hilo ataona kwamba ni sehemu ya benki hivyo hataweza kuingia ,na wao kukosa wateja.
Naye mpangaji mwingine ,mama Kalgendo alisema kuwa kitendo cha benki hiyo kubandika vibao milangoni kwa kila ofisi ni unyanyasaji kwani hakuna mpangaji mwenzako anayeruhusiwa kukubughudhi kwa kila hali ,lazima crdb wanapewa kiburi na meneja wa jengo.
Gazeti hili lilizungumza na meneja wa majengo hayo,aliyetambulika kwa jina la darius Biba ,na kusema kuwa yeye hakuwa na taarifa juu ya madai hayo ila anafanya kuyasikia tu ila atyafuatilia ikiwemo kukutana na pande zote mbili.
''kwa kweli mimi sina taarifa wewe ndiyo unanieleza ila nitakutana na pande zote mbili ili kubaini ukubwa wa tatizo hilo kwani hata hivyo vibao nafanya kuvisikia sijaviona,ila kwani hivyo vibao vinazuia nini ''alisema Bipa.
Jitihada za kumpata meneja wa tawi la benki hiyo hazikufanikiwa baada ya kuambiwa kuwa yupo kwenye kazi za nje .
Katika jengo hilo lenye wapangaji zaidi ya 30, wamedai ya kuwa ,kuna ofisi za watu mbalimbali , mashirika ya umma makampuni binafsi,kama shirika la ndege la Precision Air,ofisi za jumuia ya afrika mashariki,makampuni ya Tours,vyuo mbalimbali vinavofundisha wanafunzi,ofisi za gazeti la Arusha Times na zingine nyingi.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia